Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA-HABYARIMANA-HAKI

Rwanda: Uchunguzi wa Ufaransa ni kejeli kwa haki

Baada ya Mahakama ya Rufaa mjini Paris, nchini ufaransa, kukataa ombi la kufungua tena uchunguzi kuhusu ajali ya ndege ya rais Juvenal Habyarimana, iliyosababisha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, serikali ya Rwanda imesema uchunguzi huo ni kichekesho na unatia aibu kwa haki.

Rais wa zamani wa Rwanda Juvénal Habyarimana (hapa ilikuwa mwaka 1982).
Rais wa zamani wa Rwanda Juvénal Habyarimana (hapa ilikuwa mwaka 1982). AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Sheria, Busingye Johnston amesema kesi hiyo inayowahusisha washirika wa karibu wa Rais Paul Kagame, ilikuwa ni kejeli kwa haki na haikufaa kutokea.

Wakati huo huo shirika la waathirika wa mauaji ya kimbari, IBUKA limekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Paris. Kiongozi wa shirika hilo, Jean-Pierre Dusingizemungu, amebaini kwamba uamuzi huo ni ujumbe muhimu sana, kwa sababu "tuhuma juu ya kuhusika kwa RPF, chama cha rais Paul Kagame, ni kama kukipaka tope chama hicho", amesema, na kuongeza kuwa hii ingesababisha mvutano zaidi na kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Rwanda.

Katika mahojiano ya kila wiki ya Jeune Afrique siku zilizopita, Paul Kagame alisema "kufungua tena kesi hiyo ni kutaka kuzua matatizo. Ikiwa mambo haya hayatawekwa wazi, uhusiano wetu unaweza kuharibika kwa njia moja au nyingine," alionya.

Rais Juvenal Habyarimana aliuawa na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira katika shambulio dhidi ya ndege yao wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kanombe jijini Kigali ikitokea nchini Tanzania katika mazungumzo ya kusaka amani nchini Rwanda, Aprili 6, 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.