Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-HABYARIMANA-HAKI

Mahakama ya Ufaransa yatathmini rufaa dhidi ya kufutwa kwa kesi ya mauaji ya Habyarimana

Mahakama ya Ufaransa tangu Jumatano hii Januari 15 inatathmini rufaa dhidi ya kufutwa kwa mashitaka katika kesi ya shambulio dhidi ya ndege ya rais Juvénal Habyarimana, ambalo lilisababisha kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwezi Aprili 1994.

Eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali, usiku wa  Aprili 6 mwaka 1994
Eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali, usiku wa Aprili 6 mwaka 1994 © Getty/Scott Peterson
Matangazo ya kibiashara

Kesi kuhusu "mauaji na kula njama katika ushirikiano na kundi la kigaidi" ilifunguliwa nchini Ufaransa mnamo mwaka 1998, kufuatia mashitaka yaliyotolewa na familia za raia wa Ufaransa waliokuwa wafanyakazi wa ndege ya rais iliyodunguliwa kwa kombora mapema Aprili 6, 1994 ikijaribu kutuwa katika uwanja wa ndege kimataifa wa kanombe jijini Kigali, nchini Rwanda.

Katika ndege hiyo alikuwemo rais wa Rwanda

Juvénal Habyarimana na rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira na wasaidizi wao wengine, ambao wote walifariki dunia katika tukio hilo.

Majaji wawili wa Ufaransa wa kitengo kinachopambana dhidi ya ugaidi waliokuwa wakishughulikia kesi hiyo waliamua kuachana nayo mwaka mmoja uliopita Desemba 21, 2018, "baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha", kwa mujibu wa majaji hao ambao pia wamebaini kuwepo na "hoja zinazopingana na ambazo hazikucunguzwa" kuhusiana na ushahidi uliokusanywa.

Pamoja na rufaa hii iliyoanza kuchunguzwa tangu Januari 15, familia za wahanga zinatumaini angalau ya kuanza tena kwa uchunguzi.

Mawakili wa upande wa mashitaka wanataka hasa kwamba mahakama ya Ufaransa ipate ripoti ya siri ya mwaka 2003 kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai iliyoundwa kwa ajali ya Rwanda . Kitengo cha uchunguzi cha Mahakama ya Rufaa ya Paris kitatoa uamuzi wake katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.