Pata taarifa kuu
TANZANIA-ZANZIBAR-CORONA-UCHUMI

Zanzibar yatoa masharti ya kuingia kwa wageni

Serikali ya Zanzibar nchini Tanzania, imetangaza kufungua anga lake ili kuanza kuwaruhusu watalii kuzuru katika visiwa hivyo baada ya kile inachosema maambukizi ya virusi vya Corona yamepungua.

Mji wa kitalii wa Zanzibar wa Stone Town.
Mji wa kitalii wa Zanzibar wa Stone Town. RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Utalii Mahmoud Thabit Kombo ametangaza kuondoa vikwazo kwa wageni wanaowasili katika visiwa hivyo kuwekwa kwenye karatini pamoja na Wanzanzibari wanaorejea nyumbani.

Katika hatua nyingine, rais John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa ni Mwenyezi Mungu Ndiye aliyesaidia nchi hiyo katika vita dhidi ya Corona.

Tanzania iliacha kutangaza visa vya maambukizi mwezi Aprili, hatua ambayo imekuwa ikosolewa vikali na wakosoaji wa serikali nchini humo, ukiwemo ubalozi wa Marekani nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.