Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Wananchi wa Burundi wapiga kura kumchagua rais wao mpya

Wananchi wa Burundi leo Jumatano wamepiga kura kumchagua rais na wawakilishi wengine kama wabunge katika Uchaguzi ambao umefanyika licha ya nchi hiyo kukabiliwa na janga la Corona.

Waendesha baisikeli za kukodiwa wakiwa chini ya bendera ya Burundi huko Cibitoke, moja ya wilaya za Bujumbura, Juni 22, 2015 (picha ya kumbukumbu).
Waendesha baisikeli za kukodiwa wakiwa chini ya bendera ya Burundi huko Cibitoke, moja ya wilaya za Bujumbura, Juni 22, 2015 (picha ya kumbukumbu). MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Huu ni uchaguzi ambao umewakutanisha wagombea saba wanaotafuta urais, kuchukua nafasi ya rais Pierre Nkurunziza ambaye hawanii tena baada ya kuwa madarakani kwa miaka 15.

Wachambuzi wa siasa wanasema ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala CNDD-FDD Jenerali Evariste Ndayishimiye, na kiongozi wa zamani wa waasi Agathon Rwasa, kutoka chama kikuu cha Upinzani CNL.

Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema wapiga kura zaidi ya Milioni TANO, wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu ambao utapelekea kubadilishana kwa madaraka kwa amani kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo ya Afrika ya Kati ipate uhuru mwaka 1962.

Kuelekea Uchaguzi huu, kumeshuhudiwa makabilianio kati ya wafuasi wa chama tawala na wale wa chama kikuu cha upinzani, huku kila upande ukilaumiana.

Uchaguzi huu hautakuwa na waangalizi wa kimataifa na wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotarajiwa kuwasili nchini humo, walitangaziwa kuwekwa karatini kwa siku 14 kutokana na janga la Corona na hivyo kuwaondoa katika zoezi hilo, hatua ambayo imewanfanya wachambuzi wa siasa kuhoji iwapo zoewi hilo litakuwa huru na haki.

Vituo vya kupigia vimefunguliwa saa 12 asubuhi saa za Afrika ya Kati na kufungwa saa 10 jioni, huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa mapema mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.