Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Kampeni za Uchaguzi Mkuu kuanza Burundi

Kampeni za uchaguzi Mkuu zinaanza Jumatatu hii Aprili 27 nchini Burundi. Uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Mei 20. Kampeni hiyo itamalizika Mei 17. kampeni hizi zinaanza licha ya tishio la ugonjwa wa Corona .

Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa (kushoto) na Jenerali Évariste Ndayishimiye (kulia) mgombea wa chama tawala - CNDD-FDD, ndio wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais wa Mei 20, 2020 nchini Burundi.
Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa (kushoto) na Jenerali Évariste Ndayishimiye (kulia) mgombea wa chama tawala - CNDD-FDD, ndio wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais wa Mei 20, 2020 nchini Burundi. REUTERS/AFP/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo utajumuisha uchaguzi wa wabunge, uchaguzi wa madiwani lakini pia uchaguzi wa urais.

Kwa upande wa uchaguzi wa urais, wagombea saba watajaribu kuwashawishi wapiga kura kwa muda wa wiki hizi tatu za kampeni. Jenerali Evariste Ndayishimiye, ambaye amechukuwa mikoba ya rais anaye maliza muda wake Pierre Nkurunziza, atapeperusha bendera ya chama tawala cha CNDD-FDD.

Atakabiliana na Agathon Rwasa ambaye anaonekana kuwa ndiye mpinzani mkuu, akipeperusha bendera ya chama cha CNL ambacho kilisajiliwa mwaka mmoja uliyopita kama chama cha siasa.

Pia atawania katika uchaguzi Domitien Ndayizeye, rais wa mpito kati ya mwaka 2003 na mwaka 2005, ambaye atapeperusha bendera ya muungano wa vyama Kira Burundi. Kama wagombea wengine watatu, awali Domitien Ndayizeye alikataliwa kuwania katika uchaguzi huo na Tume ya Uchaguzi (CENI), lakini alishinda kesi hiyo baada ya kukata rufaa mbele ya Mahakama ya Katiba.

Hata hivyo waangalizi wengi wanaamini kwamba uchaguzi huo hauna changamoto nyingi. "Pamoja na upinzani, tayari inajulikana kwamba mshindi anajulikana na kwamba atakuwa ni mgombea wa CNDD-FDD", amebaini Thierry Vircoulon, mratibu wa shirika linalofanya shughuli zake kwa ukanda wa Afrika ya Kati na Kusini kutoka Taasisi ya Ufaransa ya uhusiano wa kimataifa (IFRI).

"Upinzani ambao utashiriki katika uchaguzi huu kimsingi unatekeleza tu kile kinacho julikana kama kuendeleza demokrasia kwa niaba ya utawala. kwa upande wa upinzani, lengo lao ni kupata tu viti vichache katika Bunge, ili kuendeleza uwepo wao kama vyama vya siasa vinavyotambuliwa na serikali," ameongeza.

Kwa hali yoyote ile, kila mmoja wa wagombea saba na timu zyke atakuwa na fursa ya kuelezea sera yake kwa kila siku kati ya saa 6:00 asubuhi na saa 6:00 jioni.

"Kampeni ya uchaguzi nje ya kipindi hiki ni marufuku," inabainisha sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) ambayo inaweka mfumo wa kampeni hii.

Hata hivyo upinzani umeshtumu chama tawala kwa kufanya kampeni kwa muda usiokubalika, huku CENI ikifumbia macho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.