Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-DADAAB

Kenya yakiri itashindwa kuifunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab kwa wakati

Nchi ya Kenya imekiri kuwa, haitaweza kufikia makataa ya muda wa mwisho kuifunga kambi ya wakimbizi wa Somalia ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu, baada ya Somalia kushindwa kutoa hakikisho la usalama na upatikanaji wa huduma za kijamii kwa raia wake watakaorudi nyumbani. 

Kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko kaskazini mwa nchi ya Kenya.
Kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko kaskazini mwa nchi ya Kenya. AFP PHOTO/Tony KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na shirika la habari la Reuters, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Kenya, Mwenda Njoka, amethibitisha kuwa haitawezekana kwa nchi hiyo kuifunga kambi ya Dadaab mwishoni mwa mwezi huu.

Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Kenya kukiri hadharani kuwa itashindwa kuifunga kambi hiyo, kama ilivyokuwa imeahidi hapo awali kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba, itakuwa imeifunga kambi hiyo.

Wataalamu walishaonya muda mrefu kuwa, mpango wa nchi ya Kenya kuifunga kambi ya Dadaab ambayo inawahifadhi zaidi ya wakimbizi nusu milioni, kwa muda ambao ilikuwa imetangaza, usingewezekana.

Njoka amesema kuwa, kambi hiyo ambayo ni kubwa zaidi duniani, kwa sasa inawakimbizi zaidi ya laki 2 na elfu 25, idadi hii ikitofautiana na ile ambayo mashirika ya umoja wa Mataifa yalirekodi kuwa inawakimbizi zaidi ya laki 3 na elfu 50.

Sehemu ya wakimbizi wa Somalia walioa kurejea nyumbani kwa hiari.
Sehemu ya wakimbizi wa Somalia walioa kurejea nyumbani kwa hiari. unchr.org

Mashirika ya misaada yameonya kuwa, raia wengi wa Somalia wanaopatiwa hifadhi kwenye kambi hiyo, hawako tayari kurudi kwa hiari nchini mwao hadi pale hali ya usalama itakapoimarika na huduma muhimu za kijamii kupatikana kama vile shule na vituo vya afya.

Hata hivyo haya yote hayawezi kufikiwa kwa wakati, kwakuwa hadi sasa Serikali ya Somalia bado inaendelea kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabab.

"Tutaendelea kuzungumza na Serikali ya Somalia na utawala wa Jubbaland, kwa nia ya kutazama namna bora ya kuendelea kulifanya zoezi hili kwa misingi ya haki za binadamu na pengine kulifanya kuwa la haraka zaidi," alisema Njoka wakati alipokuwa kwenye eneo la mpaka wa nchi hiyo na Jubbaland.

Nchi ya Kenya ilisema itaifunga kambi hiyo kwa sababu za kiusalama, ikidai kuwa baadhi ya wanamgambo wa Al-Shabab ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo, wanahifadhiwa kwenye kambi hiyo.

Mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Somalia, akichota maji jirani na kambi ya Dadaab, jirani na mpaka wa Kenya na Somalia, 19 October, 2011
Mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Somalia, akichota maji jirani na kambi ya Dadaab, jirani na mpaka wa Kenya na Somalia, 19 October, 2011 Reuters/Thomas Mukoya

Madai haya ya Kenya hata hivyo yamekanushwa vikali na mashirika ya misaada ambayo yamesisitiza kuwa kambi ya Dadaab ni salama na hakuna wanamgambo wanaotekeleza mashambulizi kutokea kwenye kambi hiyo.

Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi ziliionya Kenya kutowarudisha kwa nguvu wakimbizi wanaohifadhiwa kwenye kambi hiyo.

Mwezi uliopita shirika la misaada ya nchini Norway pamoja na shirika la kutetea haki za binadamu la "Human Right Watch" walikosoa namna operesheni hiyo inavyofanyika, na kudai kuwa Kenya imekuwa ikitumia nguvu kuwarudisha nyumbani maelfu ya raia wanaoishi kwenye kambi hiyo.

The United Nations and Western states warned Kenya not to forcibly repatriate those who live at the U.N.-run camp. New York-based Human Rights Watch said in September some officials were putting pressure on refugees to leave.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.