Pata taarifa kuu

DRC : Niko tayari kusitisha mpango wa kuanzisha vita na Rwanda : Rais Tshisekedi

Nairobi – Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, amesema yuko tayari kusitisha mpango wake wa kuanzisha vita na jirani yake Rwanda, ili kutoa nafasi kwa jitihada zinazoendelea za kupata suluhu ya mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Aidha mkuu wa nchi ameeleza kuwa alimwambia rais Paul Kagame huko Addis Ababa kwamba ni yeye ambaye anahitaji wakutane ana kwa ana
Aidha mkuu wa nchi ameeleza kuwa alimwambia rais Paul Kagame huko Addis Ababa kwamba ni yeye ambaye anahitaji wakutane ana kwa ana © AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi, akiwaambia waandishi wa habari kuwa yuko tayari kuchukua njia ya amani.

‘‘Rwanda iliendelea kuamsha hawa M23 Nisisema hata kuamsha bali Niseme kwamba iliendelea kujificha nyuma ya M23 na ndio sababu sitaki kufanya mazungumzo na waasi.’’ alisema rais Felix Tshisekedi.

00:51

Rais Felix Tshisekedi kuhusu M23

Aidha mkuu wa nchi ameeleza kuwa alimwambia rais Paul Kagame huko Addis Ababa kwamba ni yeye ambaye anahitaji wakutane ana kwa ana iliamuulize swali kufahamu kwamba anataka nini na nchi yake na watu wake.

Matamshi yake yamekuja siku chache kupita tangu Marekani, Ufaransa na washirika wao, kuitaka Rwanda kuacha kuwasaidia waasi wa M23 na kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi wa M23 wamekuwa wakituhumiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia mashariki wa DRC.
Waasi wa M23 wamekuwa wakituhumiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia mashariki wa DRC. AP - Moses Sawasawa

Katika hatua nyingine rais Tshisekedi, amezungumzia kesi ya mwanahabari, Stanis Bujakera, ambaye ameendelea kusota jela katika kesi inayotajwa kuwa ya kisiasa na kuahidi kuitazama upya.

‘‘Vyombo vyetu vya sharia vina shida nadhani ni mwathirika wa hali hiyo, nami nimeamua kuingilia ni kweli sipendi kufanya hivyo, mniamini ninaapa sijawahi kumpigia simu jaji yeyote ninawaaminia, ninasisitiza wahakikishe haki inafuata mkondo wake kama inavyofaa.’’ Alieleza rais Tshisekedi.

00:39

Rais Felix Tshisekedi kuhusu Stanis Bujakera

Hotuba yake imekuja baada ya rais wa Rwanda, Paul Kagame, siku ya Alhamis kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ambapo wamejadiliana kuhusu ushirikiano wa kikanda na usalama kwenye eneo la ukanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.