Pata taarifa kuu

Msani Zuchu aomba radhi kwa mamlaka visiwani Zanzibar

Nairobi – Mwimbaji maarufu nchini Tanzania Zuhura Ousmane Masud maharufu kama Zuchu, ameomba radhi baada ya mamlaka visiwani Zanzibar kumsimamisha kwa muda wa miezi sita kujihusisha na shughuli zote za kisanii katika visiwa hivyo na pia limepiga marufuku radio visiwani humo kucheza nyimbo za msanii huyo kwa kipindi cha miezi sita, kutokana na matamshi alioyatoa wakati wa onyesho lake ambalo kwa mujibu wao hayafai.

Mwanamziki toka Tanzania, Zuchu
Mwanamziki toka Tanzania, Zuchu © Zuchu - Youtube
Matangazo ya kibiashara

Onyesho la Zuchu lililojiulikana kama Fool Moon Party katika kisiwa cha Kendwa cha Zanzibar mwezi uliopita lilionyesha lugha na ishara za ngono.

Taasisi ya Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni Zanzibar Jumanne ilisema kuwa maonyesho hayo yalikwenda kinyume na mila, desturi na utamaduni wa visiwa hivyo.

Taasisi hiyo pia ilimtaka Zuchu kuwasilisha msamaha wa maandishi kueleza kuwa hatofanya tena kosa hilo, na kulipa faini ya shilingi za Kitanzania milioni moja.

Katika video iliyosambazwa kwenye mtandao wa msani huyo wa Instagram siku ya Jumanne jioni, mwanamuziki huyo aliomba msamaha kwa kosa lolote lililosababishwa na matamshi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.