Pata taarifa kuu

Nairobi na Port-Au-Prince zatia saini makubaliano ya kutuma maafisa wa polisi Haiti

Kenya na Haiti zimetia saini makubaliano siku ya Ijumaa kutuma maafisa wa polisi wa Kenya katika kisiwa hicho kilichojaa magenge kama sehemu ya ujumbe wa kimataifa unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kulingana na taarifa iliyotiwa saini na Rais wa Kenya William Ruto.

Kutokana na miito mikali kutoka kwa serikali ya Haiti na Umoja wa Mataifa, Kenya ilikubali Julai 2023 kuongoza kikosi hiki cha maafisawa polisi 2,500 hadi 2,600, kilichotarajiwa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2024.
Kutokana na miito mikali kutoka kwa serikali ya Haiti na Umoja wa Mataifa, Kenya ilikubali Julai 2023 kuongoza kikosi hiki cha maafisawa polisi 2,500 hadi 2,600, kilichotarajiwa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2024. © REUTERS/Ralph Tedy Erol
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Nchi ya Kenya na Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry, ziarani nchini Kenya, "wamejadili hatua zinazofuata ili kuruhusu kuongeza kasi ya kutumwa kwa maafisa hao wa polisi", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari ambayo haielezi kama makubaliano haya ni kinyume na uamuzi wa Mahakama ya Kenya, ambayo iliamua kinyume cha sheria mwishoni mwa mwezi Januari utumaji wa maafisa wa polisi nchini Haiti. Mkataba huo uliotiwa saini siku ya Ijumaa unatoa fursa ya kutuma maafisa wa polisi "kwa usawa".

"Ninachukua fursa hii kusisitiza kujitolea kwa Kenya kuchangia mafanikio ya misheni hii ya kimataifa. Tunaamini kuwa hili ni jukumu la kihistoria, kwa sababu amani nchini Haiti ni jambo muhimu na zuri kwa ulimwengu kwa ujumla," amesema Rais Ruto katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kutokana na wito wa kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa serikali ya Haiti na Umoja wa Mataifa, Kenya ilikubali mwezi wa Julai 2023 kuongoza kikosi hiki cha maafisa wa polisi 2,500 hadi 2,600, wanaotarajiwa "katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2024", kulingana na naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti. Umoja wa Mataifa uliidhinisha mwezi Oktoba kikosi hiki, ambacho pia kinaungwa mkono na Marekani.

kwa kikosi hiki, kabla ya kuzuiwa na uamuzi wa mahakama. Serikali ilitangaza nia yake ya kukata rufaa. Mpinzani Ekuru Aukot, ambaye aliwasilisha malalamiko dhidi ya kutumwa kwa kikosi hiki, ameliambia shirika la habri la AFP siku ya Ijumaa kwamba atawasilisha malalamishi "kwa kudharau mahakama".

Mwezi wa Januari 2024 ulikuwa "wa vurugu zaidi katika zaidi ya miaka miwili" nchini Haiti, kulingana na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, ambaye anasikitika kwamba "hali ambayo ni mbaya" "imezorota zaidi, katika muktadha wa kuendelea na kuongezeka kwa vurugu za magenge.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.