Kenya: Mahakama yatia breki mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu
Nairobi – Mahakama ya rufaa nchini Kenya, imeamua kuwa mpango wa utozwaji kodi unaotekelezwa na serikali ya rais William Ruto ili kujenga makaazi yenye bei nafuu, ni kinyume cha sheria.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Serikali ilikuwa imeiomba mahakama kuiruhusu kuendelea kutoza ushuru huo kutoka kwa mapato ya kila mwezi kutoka kwa raia walioajiriwa wakati ikisubiri kusikizwa kwa rufaa ya kupinga mpango huo wa utawala wa rais Ruto.
Mwezi Juni mwaka uliopita, Rais William Ruto alitia saini sheria ya fedha ya mwaka wa 2023, sheria ambayo imepingwa na baadhi ya raia na upinzani.
Kwa mujibu wa sheria hiyo raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki wamekuwa wakikatwa asilimia 1.5, makato yanayolipwa kila mwezi na waajiri na wafanyikazi.
Mwezi Novemba,Mahakama ya Juu iliamua kwamba ushuru huo ulikuwa kinyume na katiba na kuizuia serikali kutekeleza mpango huo.
Serikali imetetea sheria hiyo ikisema kuwa inalenga kuwajengia raia wake wenye kipato cha chini nyumba za bei nafuu pamoja na kuunda nafasi za ajira.
Wakenya wamepata ahueni ya muda japokuwa Mahakama ya Rufaa bado haijatoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu sheria hiyo.
Uamuzi huo unakuja wiki moja baada ya mahakama ya rufaa kutoa idhini ya kutozwa ada ya bima ya afya yenye utata, ambayo itahitaji raia wa Kenya kuchangia asilimia 2.75 ya mishahara yao ya kila mwezi kwa mpango wa afya ya kijamii.
The 220 units project will create more than 4,000 jobs, including the local Jua Kali that will be tasked with producing 1,200 doors costing at least Sh26 million.
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) January 16, 2024
Deputy President @rigathi, Cabinet Secretaries @WahomeHon, Ezekiel Machogu, Nandi Governor @Araap_Sang, MPs and MCAs… pic.twitter.com/GtzSz7E8TW