Pata taarifa kuu

Kenya : Mahakama inataka kikao na mkuu wa nchi kuhusu vitisho dhidi yake

Nairobi – Jaji Mkuu nchini Kenya, Martha Koome amesema mahakama imemwandikia barua rais William Ruto, barua ambayo inamtaka mkuu wa nchi kujadili na uongozi wa idara hiyo kuhusu madai aliyoyatoa dhidi ya baadhi ya majaji.

Mkuu wa nchi amekuwa akiwatuhumu baadhi ya majaji na idara ya mahakama kwa kushirikiana na upinzani kuyumbisha miradi ya serikali
Mkuu wa nchi amekuwa akiwatuhumu baadhi ya majaji na idara ya mahakama kwa kushirikiana na upinzani kuyumbisha miradi ya serikali AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto katika siku za hivi karibuni, ameonekana kuishambulia idara ya mahakama kwa kile anachosema kuwa baadhi ya majaji ni wafisadi na wanashirikiana na upinzani kuhujumu miradi ya serikali yake.

Akizungumza na vyombo vya habari kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki siku ya Jumatatu, jaji mkuu Martha Koome alieleza kuwa hatua ya kushambuliwa kwa idara ya mahakama na wanasiasa inaelekeza nchi hiyo katika njia mbaya na mzozo wa kikatiba.

Naye kinara upinzani kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki Raila Odinga, amemtuhumu rais Ruto kwa kujaribu kuwatisha majaji.

Chama cha mawakili kiliandaa maandamano wiki iliyopita kulaani kile walichosema ni hatua ya mkuu wa nchi kuishambulia idara ya mahakama.

Rais Ruto aliyeingia madarakani mwaka wa 2022, amekuwa akituhumiwa kwa kuwaongezea ushuru mkubwa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki haswa wakati huu wanapkabiliwa na kupanda kwa gharama ya maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.