Pata taarifa kuu

Rais wa Belarus ziarani nchini Kenya kuimarisha uhusiano wa kibiashara

Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, mshirika mwaminifu wa Moscow na anayetengwa na nvhi za Magharibi, amekutana na mwenzake wa Kenya William Ruto siku ya Jumatatu mjini Nairobi ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ofisi ya rais wa Kenya imetangaza.

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko anaongoza mkutano na maafisa wa kijeshi huko Minsk, Belarus, Februari 24, 2022.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko anaongoza mkutano na maafisa wa kijeshi huko Minsk, Belarus, Februari 24, 2022. © Nikolay Petrov/BelTA/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Belarus alianza ziara barani Afrika siku ya Jumamosi, baada ya kukutana na Rais wa Equatorial Guinea Téodoro Obiang Nguema huko Malabo. Ziara hii inalenga kuendelea kuanzisha "uhusiano wa karibu" kati ya Minsk na nchi za Afrika.

Kufuatia majadiliano kati ya William Ruto na Alexander Lukashenko, nchi hizo mbili zimetangaza kwamba zinataka kuimarisha "uhusiano wao katika nishati mbadala, biashara, uwekezaji na elimu", amebainisha Bw. Ruto kwenye mtandao wa X. Rais wa Kenya pia amesisitiza kuwa nchi hiyo "ina nia hasa ya kutumia teknolojia ya juu ya kilimo ya nchi hii ya Ulaya Mashariki ili kuongeza tija yake."

Alexander Lukashenko amesalia madarakani kwa miaka 29, na nchi hiyo mara nyingi hujikuta ikitengwa na washirika wa Magharibi na kulengwa kwa vikwazo vikali kwa ukandamizaji wake wa upinzani na uungaji mkono wake kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alitembelea Kenya mwezi Mei, nchi yenye nguvu kiuchumi Afrika Mashariki.

Moscow na Kyiv wanataka kuongeza ushawishi wao katika bara la Afrika. Mwezi Februari, nchi 22 kati ya 54 wanachama wa Umoja wa Afrika zilijizuia au hazikushiriki katika kupigia kura azimio la hivi punde la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linaloitaka Urusi kuondoa majeshi yake nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.