Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Sudan Kusini: Rais Salva Kiir akutana kwa mazungumzo na Vladimir Putin mjini Moscow

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir aliwasili Moscow jioni ya Jumatano, Septemba 27, kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili. Katika ajenda ya majadiliano baina ya nchi hizo mbili, kuimarika kwa uhusiano wa ushirikiano wa kiusalama kati ya Sudan Kusini na Urusi. Ushirikiano pia katika nyanja za elimu, afya na maendeleo ya kiuchumi. Juba inatumai zaidi kupata uungwaji mkono wa Urusi kwa vikwazo vya silaha vitakavyoondolewa hivi karibuni na Baraza la Usalama.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alikutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow mnamo Septemba 28, 2023.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alikutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow mnamo Septemba 28, 2023. AFP - VLADIMIR ASTAPKOVICH
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux

Siku chache zilipita Salva Kiir akirejea kutoka New York, ambako alishiriki katika Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, na kuondoka kwake kuelekea Moscow. Ishara ya mvutano kati ya Sudan Kusini na Marekani, Salva Kiir hakukutana na Joe Biden wakati wa ziara yake nchini Marekani. Kwa upande mwingine, alipokelewa kwa shangwe huko Moscow.

Akiwa ameandamana na ujumbe mkubwa pamoja na Waziri wake wa Mambo ya Nje na maafisa kadhaa wakuu wa usalama, rais wa Sudan Kusini alielezea matakwa yake ya kuimarisha uhusiano na Moscow. Kutoka dakika za kwanza za mkutano wake na Putin, Salva Kiir alitangaza kwamba "hakuwa na njia mbadala" na aliiona Urusi ya Vladimir Putin "rafiki mkubwa" ambayo "anaihitaji".

Rais wa Sudan Kusini anatumai hasa kunufaika ndani ya miezi michache kutokana na uungwaji mkono wa Urusi katika Umoja wa Mataifa ili kuiondolea vikwazo vya silaha. Urusi inatafuta washirika wapya wa kijiografia na kisiasa huku kukiwa na vita nchini Ukraine. Tayari inawekeza katika uchimbaji wa mafuta nchini Sudan Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.