Pata taarifa kuu

Rais wa Sudan Kusini anazuru Moscow

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir yuko jijini Moscow kwa mazungumzo na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Ziara hiyo inalenga pia kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa yao pamoja na kuangazia ushirikiano katika sekta ya biashara na usalama.
Ziara hiyo inalenga pia kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa yao pamoja na kuangazia ushirikiano katika sekta ya biashara na usalama. AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inakuja wakati huu Urusi na mataifa ya Magharibi yakiwa mbioni kujaribu kutafuta uungwaji mkono wa bara Afrika, vita vya Ukraine vikiendelea.

Rais Kiir aliwasili katika mji mkuu wa Urusi siku ya Jumatano na kupokelewa na naibu waziri wa mambo ya kigeni Andrey Rudenko Yurevich, kwa mujibu wa taarifa kutoka katika idara ya mawasiliano ya rais.

Afisi ya rais Kiir inasema mkutano huo kati yake na rais wa Urusi utajadili kuhusu uwezekano wa maendeleo na uhusiano katika nyanja tofauti ikiwemo ya kimataifa.

Taarifa hiyo inasema ziara hiyo inalenga pia kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa yao pamoja na kuangazia ushirikiano katika sekta ya biashara na usalama.

Viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili hatua ya kuondolewa kwa marafuku ya ununuzi wa silaha na vikwazo vingine vinavyo walenga baadhi ya raia wa Sudan Kusini, taarifa hiyo iliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.