Pata taarifa kuu

Joe Biden: Ulimwengu unatiwa wasiwasi na sheria hii 'dhidi ya ushoga' nchini Uganda

Tangazo la kuidhinishwa kwa sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja na "kukuza" ushoga nchini Uganda Mei 29, linaibua hasira na wasiwasi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani hadi Ikulu ya White House, nchini Marekani.

Ofisi ya rais wa Uganda ilitangaza kwamba mkuu wa nchi, Yoweri Museveni, "ameidhinisha" nakala hii, ambayo "sasa inakuwa sheria ya kupinga ushoga 2023".
Ofisi ya rais wa Uganda ilitangaza kwamba mkuu wa nchi, Yoweri Museveni, "ameidhinisha" nakala hii, ambayo "sasa inakuwa sheria ya kupinga ushoga 2023". AP
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais wa Uganda ilitangaza kwamba mkuu wa nchi, Yoweri Museveni, "ameidhinisha" nakala hii, ambayo "sasa inakuwa sheria ya kupinga ushoga 2023".

Habari hiyo ilizidisha hofu iliyozushwa mwezi Machi kutokana na kura ya awali ya mswada huo, ambayo  Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu (OHCHR), Volker Türk, ameita wakati huo "nakala ya kibaguzi - mbaya zaidi ya aina yake duniani".

'Shambulio kali dhidi ya haki za binadamu'

Siku ya Jumatatu OHCHR imesema "imesikitishwa" kuona mswada huu "wa kibaguzi na wa kikatili" ukianza kutumika, "kinyume na Katiba na mikataba ya kimataifa", ambayo inafungua njia ya "ukiukwaji wa utaratibu wa haki za watu kutoka jamii ya LGBT".

Rais wa Marekani Joe Biden, akilaani "ukiukwaji mbaya" wa haki za binadamu, ameomba idara zake kuchunguza matokeo ya sheria hii juu ya "mambo yote ya ushirikiano kati ya Marekani na Uganda", hasa misaada na uwekezaji, kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Marekani.

Naibu mkurugenzi wa Afrika wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, Ashwanee Budoo-Scholtz, amechukizwa na "sheria ya kibaguzi" na "hatua moja katika mwelekeo mbaya". Shirika la kimataifa la Haki za Bindamu la Amnesty International limelaani "sheria kandamizi" ambayo ni "shambulio kubwa dhidi ya haki za binadamu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.