Pata taarifa kuu

Kenya yarusha satelaiti yake ya kwanza angani

Satelaiti ya kwanza ya Kenya kufanya kazi iliwekwa kwenye obiti Jumamosi na roketi ya SpaceX iliyopaa kutoka California (Marekani), kulingana na picha kutoka kwa kampuni ya anga ya Marekani.

Wahandisi wa Shirika la Anga la Kenya (KSA) Aloyce Were (kushoto), Deche Bungule (C) na Andrew Nyawade ambao walitengeneza satelaiti ya kwanza ya Kenya ya Taifa-1 inayofanya kazi.
Wahandisi wa Shirika la Anga la Kenya (KSA) Aloyce Were (kushoto), Deche Bungule (C) na Andrew Nyawade ambao walitengeneza satelaiti ya kwanza ya Kenya ya Taifa-1 inayofanya kazi. © Simon MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uzinduzi huo uliopangwa kufanyika Jumatatu jioni nchini Marekani, uliahirishwa mara kadhaa wiki hii kutokana na hali mbaya ya hewa.

Siku ya Jumamosi, roketi ya SpaceX Falcon-9 iliruka saa 06:48 GMT kutoka kituo cha Marekani huko Vandenberg (California), kabla ya kupeleka satelaiti kadhaa saa moja baadaye, ikiwa ni pamoja na Taifa-1 ya Kenya.

Ikiwa imeundwa na kuendelezwa na timu ya watafiti wa Kenya, satelaiti hii inapaswa kutoa data katika nyanja za kilimo na ufuatiliaji wa mazingira nchini Kenya, muhimu kwa mustakabali wa nchi hii ya Afrika Mashariki ambayo kwa sasa inakabiliwa na ukame wa kihistoria.

Katika taarifa ya pamoja, Wizara ya Ulinzi ya Kenya na Shirika la Anga za Juu la Kenya (KSA) wiki jana walipigia debe "hatua muhimu" ambayo inapaswa kutoa msukumo kwa "uchumi changa wa anga za juu wa Kenya".

"Tunanufaika moja kwa moja na uchunguzi wa anga, tutaweza kuboresha usalama wetu wa chakula," Pattern Odhiambo, mhandisi katika KSA, ambaye alishiriki katika mradi huo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa picha kutoka kwa kamera ya satelaiti yenye spectra mbalimbali, "tutaweza kuwa na data ya hali ya juu ya uchunguzi wa ardhi, ambayo itatusaidia kutabiri mavuno ya mazao," ameongeza.

Kenya ilituma satelaiti yake ya kwanza ya nano angani mwaka wa 2018.

Kufikia 2022, zaidi ya satelaiti 50 za Kiafrika zimetumwa angani, kulingana na Space in Africa, kampuni ya Nigeria inayofuatilia programu za anga za Afrika.

Misri ilikuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kutuma satelaiti angani mwaka 1998.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.