Pata taarifa kuu

Kenya kurusha satelaiti yake ya kwanza kufanya kazi tarehe 10 Aprili

Kenya itarusha satelaiti yake ya kwanza angani nchini Marekani mnamo Aprili 10 pamoja na kampuni ya Marekani ya SpaceX, Wizara ya Ulinzi ya Kenya na Shirika la Anga za Juu la Kenya zimetangaza Jumatatu.

Picha hii inaonyesha mfululizo wa kundi la setilaiti za SpaceX Starlink zikipita juu ya anga ya Uruguay mnamo Februari 7, 2021.
Picha hii inaonyesha mfululizo wa kundi la setilaiti za SpaceX Starlink zikipita juu ya anga ya Uruguay mnamo Februari 7, 2021. © AFP/Mariana Suarez
Matangazo ya kibiashara

Satelaiti hii "itatoa data sahihi na ya kawaida ya satelaiti" ambayo itakuwa muhimu hasa katika "maeneo ya kilimo na usalama wa chakula, usimamizi wa maliasili na majanga na ufuatiliaji wa mazingira", kulingana na taarifa.

Kenya, nchi yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki, imeathiriwa na ukame wa kihistoria, baada ya misimu kadhaa ya mvua kushindwa. Satelaiti hiyo, Taifa-1, “iliundwa na kutengenezwa na timu ya watafiti wa Kenya,” taarifa hiyo imeongeza.

Uzinduzi huo utakaofanyika kutoka kituo cha Marekani cha Vandenberg, California, kwa kutumia roketi ya SpaceX Falcon 9, ni "hatua muhimu kwa mpango wa anga za juu wa Kenya na unatarajiwa kuchangia pakubwa katika kuchochea ukuaji wa maendeleo ya satelaiti, uchambuzi na usindikaji wa data na uwezo wa maendeleo ya matumizi ya uchumi wa anga za juu wa Kenya," Wizara ya Ulinzi na Shirika la Anga la Kenya zimesema.

Mnamo 2018, Kenya ilituma satelaiti yake ya kwanza ya nano. Kufikia mwaka 2022, angalau nchi 13 za Afrika zilikuwa zimetengeneza satelaiti 48, kulingana na Space in Africa, kampuni ya Nigeria inayofuatilia programu za anga za Afrika. Misri ilikuwa nchi ya kwanza barani humo kutuma satelaiti angani mwaka 1998.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.