Pata taarifa kuu

Papa awasili Kinshasa, ikiwa ni hatua ya kwanza ya ziara yake barani Afrika

Kiongozi wa kanisa Katolika duniani, Papa Francis, amewasili mjini mku wa DRC, Kinshasa, kwa ndege leo Jumanne kwa ziara ya siku nne nchini humo, nchi iliyokumbwa na ghasia zilizoenea, hatua ya kwanza ya safari ambayo itampeleka hadi Sudan Kusini.

Bango la kumkaribisha Papa Francis ambaye yuko Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Januari 31 hadi Februari 3, 2023. Hapa mbele ya makao makuu ya CENCO mjini Kinshasa (Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa DRC).
Bango la kumkaribisha Papa Francis ambaye yuko Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Januari 31 hadi Februari 3, 2023. Hapa mbele ya makao makuu ya CENCO mjini Kinshasa (Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa DRC). © Véronique Gaymard/RFI
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya papa iliondoka Roma saa 8:28 asubhi (sawa na saa 8:28 saa za Afrika ya Kati) na ilitakiwa kutua mwendo wa saa Tisa alaasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kinshasa, mji mkuu wa nchi hii kubwa zaidi yenye Wakatolika wengi barani Afrika. , ambapo atakaribishwa kwa shangwe, kwani wengi wanamsubiri kwa hamu.

Mapema mchana, wakazi wachache wa Kinshasa walianza kukusanyika mbele ya uwanja wa ndege, na kufuatiwa kwa muda wa saa na umati wa watu waliozidi kuwa wengi na kusubiri kumwona kwenye gari lake "papamobile", ambayo itapeleke katikati ya jiji, kama umbali wa kilomita 25.

"Sikutaka kukosa fursa hii ya kuonana naye ana kwa ana," Maggie Kayembe, mwenye umri wa miaka thelathini, ameliambia shirika la habari la AFP. “Siku zote anahubiri amani popote anapoenda, na amani, tunaihitaji sana,” ameongeza mwanamke huyo.

ziara hii ambayo hapo awali ilipangwa kufanyika mwezi Julai 2022,  iliahirishwa kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata papa mwenye umri wa miaka 86, ambaye anasafiri kwa kiti cha magurudumu, lakini pia hatari za kiusalama huko Goma, mashariki mwa nchi, ziara ambayo hatimaye ilifutwa.

Kwa ziara yake ya arobaini ya kimataifa tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2013, ikiwa ni ya tano katika bara la Afrika, Mjesuiti wa Argentina anatarajia kutoa wito wa wa kusitishwa kwa mapigano katika nchi hii iliyokumbwa na ghasia mbaya na ambapo theluthi mbili ya takriban wakazi milioni 100 wanaishi kwa zaidi ya dola 2.15 kwa siku.

DRC inakabiliwa na kuibuka tena kwa kundi la waasi la M23 ambalo katika miezi ya hivi karibuni limeteka maeneo makubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini, mkoa wa DRC unaopakana na Rwanda ambayo Kinshasa naituhumu kuingilia masuala ya ndani ya chi hiyo.

Mashariki mwa DRC pia ina makumi ya makundi yenye silaha, wakiwemo waasi wa Kiislamu wanaolenga raia. Ziara hii pia inajiri wiki mbili baada ya shambulio la umwagaji damu lililodaiwa na kundi la Islamic State (IS) katika kanisa la Kipentekoste huko Kivu Kaskazini.

Papa kupokelewa na Tshisekedi

Baada ya hafla ya kukaribishwa katika uwanja wa ndege, mkuu wa Kanisa Katoliki atakwenda Ikulu ya taifa, ambako atapokelewa na Rais Felix Tshisekedi. Kisha atatoa hotuba ya kwanza mbele ya mamlaka, mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

"Hotuba hii itawagusa wengi, atatoa ujumbe mzito kwa wanasiasa kwa kushughulikia suala la rushwa", hasa kwa kuzingatia uchaguzi mkuu utakaofanyika mwxezi Desemba, anasisitiza Samuel Pommeret, meneja wa mradi katika shirika lisilo la kiserikali la CCFD Terre Solidaire katika kanda ya Maziwa Makuu.

Misa kubwa kufanyika kabla ya mkesha wa maombi

Jumanne jioni, makumi ya maelfu ya watu wanatarajiwa kushiriki katika mkesha wa maombi katika uwanja wa ndege wa N'dolo wa Kinshasa, ambapo watalala usiku, kabla ya misa kubwa Jumatano asubuhi ambapo zaidi ya waumini milioni moja wanatarajiwa.

Katika siku za hivi karibuni, maandalizi yameongezeka katika mji mkuu wa Kongo, ambapo mabango na paneli kubwa hushindana na jumbe za kumkaribisha papa wa kwanza kuzuru nchi hiyo tangu John Paul II mwaka 1985.

Wakati wa ziara yake katika nchi hii kubwa ambapo Kanisa lina nafasi kubwa katika jamii na siasa, Francis pia atakutana na wahanga wa ghasia, wakleri na wawakilishi wa mashirika ya misaada.

Katika hotuba zake kiongozi huyo wa Wakatoliki bilioni 1.3 anapaswa kuzungumzia pamoja na mambo mengine changamoto ya ongezeko la joto duniani na ukataji miti, elimu, masuala ya kijamii na kiafya na msaada kwa jumuiya ya Kikristo.

Siku ya Ijumaa, atasafiri kwenda Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, taifa changa zaidi duniani na miongoni mwa mataifa maskini zaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.