Pata taarifa kuu

Mahakama ya Juu kutoa uamuzi kuhusu Matokeo ya Uchaguzi Kenya

Mahakama ya Juu nchini Kenya inatarajia kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita iliyowasilishwa na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga.

Waziri mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kushoto) na aliyekuwa makamu wa rais wa muungano wa Kenya Kwanza na rais mteule William Ruto (kulia).
Waziri mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kushoto) na aliyekuwa makamu wa rais wa muungano wa Kenya Kwanza na rais mteule William Ruto (kulia). AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Agosti 15, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilimtangaza Dkt Ruto kuwa Rais mteule baada ya kupata kura milioni 7,176,141 aliyepata asilimia 50.49 dhidi ya milioni 6,942,930 za Bw Odinga, ambaye alipata asilimia 48.85).

Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi huo na ambaye aliwasilisha mahakamani malalamiko yake anasema kura hiyo ilibadilishwa ili kumpa mpinzani wake William Ruto ushindi mwembamba katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali. Mawakili wa Bw Ruto na tume ya uchaguzi wanakanusha madai hayo.

Bw Odinga, kwa upande mwingine, anaamini kuwa uchaguzi wa urais wa Agosti 9 ulikumbwa na dosari nyingi, akiongeza kwamba alichokuwa akitafuta ni "ukweli" tu na kwamba angerejea nyumbani ikiwa angepoteza uchaguzi huo kwa haki.

Wagombea wote wawili wameahidi kuheshimu uamuzi wa mahakama kuu.

Uamuzi wa Jumatatu unaweza kubadilisha hali ya kisiasa ya nchi na pia kutoa fursa ya kurekebisha sheria za uchaguzi za nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.