Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais Kenya: Mahakama ya Juu kutoa uamuzi Septemba 5

Mahakama ya Juu nchini Kenya imetangaza Jumanne kuwa imebakisha masuala tisa ambayo yatajadiliwa katika rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9, ikiwa ni pamoja na tuhuma za udanganyifu uharamia ambao unaweza kusababisha kura hiyo kubatilishwa.

Waziri mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kushoto) na aliyekuwa makamu wa rais wa muungano wa Kenya Kwanza na rais mteule William Ruto (kulia).
Waziri mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kushoto) na aliyekuwa makamu wa rais wa muungano wa Kenya Kwanza na rais mteule William Ruto (kulia). AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais William Ruto alitangazwa mshindi na Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC), akiongoza kwa takriban kura 233,000 (50.49% dhidi ya 48.85%) alizopata Raila Odinga, kiongozi wa kihistoria wa upinzani mwenye umri wa miaka 77 anayeungwa mkono na chama tawala.

Mgombea urais kwa mara ya tano, Odinga amelaani udanganyifu na kuwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu. Rufaa zingine nane ziliwasilishwa na watu binafsi na mashirika, mbili kati yao zilitupiliwa mbali.

Siku ya Jumanne, Mahakama ya Juu imesema itazingatia masuala tisa katika usikilizwaji wa kesi inayotarajiwa kuanza Jumatano, kabla ya uamuzi wake unaotarajiwa Septemba 5.

Majaji saba wananuia kutathmini iwapo teknolojia ya uchaguzi, iliyotumiwa hasa kufuatilia matokeo kutoka vituo vya kupigia kura hadi kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura, ilikidhi "viwango vya uadilifu, uthibitisho, usalama na uwazi".

Makosa katika mfumo wa kielektroniki yalipelekea Mahakama ya Juu kufutilia mbali uchaguzi uliopita wa urais wa Agosti 2017 - wa kwanza barani Afrika - baada ya Raila Odinga kukata rufaa.

Siku ya Jumanne mahakama imeamuru IEBC kumpa Raila Odinga na walalamishi wengine idhini "kamili na usiozuiliwa" kutazama seva za kompyuta zilizotumiwa kwa uchaguzi. Bw Odinga alidai hasa kwamba wavamizi walivamia seva na kuzipakia fomu za matokeo ya uchaguzi ya uongo, madai ambayo rais wa IEBC alikanusha.

Pia alisema kuwa matokeo katika angalau vituo 14 kati ya 46,000 yanapaswa kupitiwa na kuhesabiwa upya.

Baada ya kutathmini uwazi wa kura hiyo, itabainisha iwapo William Ruto amefikia kiwango cha kikatiba cha 50% pamoja na kura moja kutangazwa kuchaguliwa katika duru ya kwanza.

Tangu mwaka wa 2002, chaguzi zote za urais nchini Kenya zimekuwa zikipingwa, wakati mwingine kusababisha ghasia za baada ya uchaguzi.Machafuko ambayo yalisababisha zaidi ya 1.100 mwaka 2007.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, Bw. Ruto na Odinga walikuwa wameahidi kutatua tofauti zozote mahakamani badala ya mitaani.

Ikiwa Mahakama ya Juu itabatilisha uchaguzi huo, ni lazima kura mpya ifanyike ndani ya siku 60. Iwapo itathibitisha matokeo hayo, William Ruto atakuwa rais wa tano wa Kenya tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1963.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.