Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa Rais nchini Kenya: Mvutano waageuka kuwa mazungumzo ya viziwi

Siku ya Jumatano Agosti 17, Raila Odinga na muungano wake walithibitisha kwamba watawasilisha rufaa mbele ya Mahakama ya Juu kupinga ushindi wa William Ruto uliotangazwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jumatatu. Wakati huo huo, William Ruto aliwasilisha vipaumbele vya serikali yake ijayo mbele wabunge na maseneta kutoka muungano wake.

Waziri mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kushoto) na aliyekuwa makamu wa rais wa muungano wa Kenya Kwanza na mgombea urais William Ruto (kulia).
Waziri mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kushoto) na aliyekuwa makamu wa rais wa muungano wa Kenya Kwanza na mgombea urais William Ruto (kulia). AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Kambi y a Raila Odinga inajipanga. Jumatano hii, wawakilishi waliochaguliwa wa muungano wake waliidhinisha kuwasilishwa kwa rufaa katika Mahakama ya Juu kujaribu ushindi wa William Ruto ubatilishwe. Msisitizo: tusikate tamaa na tuendelee licha ya kile kilichotokea, alisema Martha Karoua, mgombea mwenza wa Raila Odinga. “Ushindi wetu umechelewa, lakini utakuja. Na huu ni ujumbe kwa kila mtu. Asante kwa uungwaji wenu mkono. Hatutawaangusha. "

Wakati huo huo, William Ruto, alivaa vazi la urais katika hotuba kwa maafisa waliochaguliwa wa muungano wake. Hakutaja jina la Raila Odinga na alitaja kwa ufupi tu kuwania uchaguzi wake. Mkakati wake: kusonga mbele na kuonyesha kwamba tayari anajionyesha katika hatua ya serikali yake ya baadaye.

“Matarajio ya watu wa Kenya ni makubwa na hatuwezi kumudu anasa ya kupoteza muda. Hivi karibuni, mara tu mchakato utakapokamilika, tutachukua hatua za kuhakikisha tunaendesha serikali yenye uwazi, kidemokrasia na inayowajibika.”

William Ruto pia aliahidi kuwa uongozi wake utavuka mipaka ya kikabila na kuapa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanahudumia "Wakenya wote kwa usawa", bila kujali "kabila" zao au "misimamo ya kisiasa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.