Pata taarifa kuu

Kenya: Mfahamu Raila Odinga, mwanasiasa mkongwe

Wafuasi wake kwa upendo humwita "baba", kwa Kiswahili. Akiwa na umri wa miaka 77, Raila Amolo Odinga ni mkongwe wa siasa za Kenya. Mgombea urais wa Agosti 9, hii ni mara ya tano kwa yeye kujaribu kuwania kwenye nafasi hii.

Raila Odinga wakati wa kurasimishwa kuwa mgombea wa urais wa Kenya mnamo Desemba 10, 2021 jijini Nairobi.
Raila Odinga wakati wa kurasimishwa kuwa mgombea wa urais wa Kenya mnamo Desemba 10, 2021 jijini Nairobi. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa upinzani, na aliweza kuchukuwa nafasi mbalimbali katika serikali, "nyayo zake zinaonekana katika eneo zima la kisiasa la Kenya", amebaini mchambuzi wa kisiasa Dismas Mokua. Katika maisha yake ya muda mrefu katika siasa, amejenga msingi wa uungwaji mkono wa uaminifu na usio na masharti, hasa miongoni mwa Wajaluo, jamii iliyoko magharibi mwa Kenya ambako anatoka.

Ikiwa atakanusha leo, Raila Odinga anachukuliwa kuwa sehemu ya "nasaba" hizi za kisiasa za Kenya. Baba yake, Jaramogi Oginga Odinga alikuwa makamu wa rais chini ya utawala wa Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya baada ya uhuru na baba wa rais wa sasa, Uhuru Kenyatta.

Wakati wa kampeni, alijaribu kujiweka kama baba, karibu na watu, kwa kutetea hatua za kijamii kama vile "Baba care", zinazopaswa kutoa huduma za afya za bei nafuu kwa wote, au kuanzisha msaada wa kifedha wa kila mwezi wa Shilingi 6,000 za Kenya (sawa na euro 48) kwa familia zilizo hatarini zaidi. Pia alitangaza nia yake ya kujadili msamaha wa madeni na kuweka vita dhidi ya ufisadi katika kiini cha mpango wake.

Baadhi humuita mtu anayependwa na watu wengi, wengine "msoshalisti", wakirejelea hasa masomo yake ya uhandisi huko Ujerumani Mashariki ya kikomunisti au jina la kwanza la mtoto wake mkubwa Fidel, kwa kumuenzi Fidel Castro, lakini Odinga pia anaongoza urithi thabiti wa kiuchumi, anafanya biashara hasa katika sekta ya ethanoli na petroli.

Kujihusisha kwake kisiasa kulianza mwanzoni mwa miaka ya 1980 alipofanya kampeni dhidi ya utawala wa chama kimoja uliokuwa ukitumika wakati huo nchini Kenya, ambao ulimfanya azuiliwe kwa miaka kadhaa. Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1982, akishukiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi dhidi ya Daniel Arap Moi, Rais wa Kenya wakati huo. Alikaa gerezani kwa miaka sita kabla ya kuachiliwa mnamo mwezi Februari 1988, kisha kushikiliwa tena mara ya pili. Hatimaye alienda uhamishoni kwa muda mfupi huko Norway.

Aliporudi nchini Kenya mnamo 1992, hakuacha siasa na aliingia Bungeni. Kulifuata miongo kadhaa ya upinzani ambapo aligombea urais, lakini alishindwa mara nne, mnamo mwaka 1997, 2007, 2013 na 2017.

Waziri Mkuu kutoka 2008 hadi 2013

Mnamo 2005, Odinga aliamua kuunda chama chake cha kisiasa, Orange Democratic Movement (ODM), ambacho chini ya bendera yake alikuwa mgombea wa urais mnamo 2007, ambapo Mwai Kibaki aliibuka mshindi. Matokeo hayo yalipingwa vikali, hasa na Odinga, kiongozi wa jamii ya Wajaluo. Wiki kadhaa za ghasia za kikabila zilifuata ambapo zaidi ya watu 1,100 walipoteza maisha na laki kadhaa kutoroka makazi yao. Martha Karua, mgombea mwenza wa sasa wa Odinga kwa kiti cha urais, wakati huo alishutumu chama chake, ODM, kwa kuchochea "uuangamizaji wa kikabila".

Mgogoro huo ulitatuliwa kwa makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Mwai Kibaki na Raila Odinga, ambaye aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu. alishikilia nafasi hiyo kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2013. Katika kipindi hiki, yeye ni mmoja wa wasanifu wa Katiba ya 2010.

Raila Odinga aligombea tena uchaguzi wa urais mwaka wa 2013 na 2017. Alishindwa mara mbili dhidi ya Uhuru Kenyatta, na kupinga matokeo mbele ya Mahakama ya Juu Zaidi. Mahakama haikukubaliana na uchaguzi huo mnamo mwaka 2013, lakini iligundua "makosa" mnamo 2017 na ikafuta uchaguzi. Uchaguzi mpya uliitishwa, lakini Raila Odinga alitoa wito wa kususia uchaguzi huo. Kenyatta alishinda kwa 98% ya kura na waliopiga kura walifikia 39%.

Odinga hakutaka kutambua matokeo ya uchaguzi na alifikia hatua ya kuandaa hafla ya kutawazwa mnamo Januari 2018 ambapo alijitangaza "Rais wa watu". Ili kumaliza mvutano huo, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga walipeana mikono mnamo mwezi Machi 2018, ishara iliyopewa jina la utani la "kushikana mikono", ambayo imekuwa ishara muhimu.

Kibaraka wa utawala, kulingana na wapinzani wake

Huu ni mwanzo wa ushirikiano wa kisiasa kati ya watu hao wawili. Kwa pamoja, walifanya kampeni ya mageuzi ya Katiba, mpango wa "Building Bridges Initiative", unaoitwa "BBI", ambao unalenga, miongoni mwa mambo mengine, kuunda wadhifa wa Waziri Mkuu. Mahakama ya Juu ilifutlia mbali na kuuita mpango huo kuwa ni kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.