Pata taarifa kuu

Ruto aidhinishwa kuwania kiti cha urais Kenya

Nchini Kenya, Tume ya Uchaguzi imemwidhinisha Naibu rais William Ruto kugombea urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti. 

William Ruto, makamu wa rais wa Kenya na mgombea wa UDA, wakati wa mkutano wa Januari 18, 2022.
William Ruto, makamu wa rais wa Kenya na mgombea wa UDA, wakati wa mkutano wa Januari 18, 2022. REUTERS - BAZ RATNER
Matangazo ya kibiashara

Baada ya hatua hiyo, Ruto ambaye wiki hii alilalamika kuwa wapiga kura karibu Milioni moja kutoka kwenye ngome zake wameondolewa kwenye daftari la kupigia kura, amesema ana imani na Tume hiyo na baadaye akaongoza kampeni ya siasa jijini Nairobi. 

Mgombea mwingine, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, anatarajiwa kuidhinishwa hapo kesho. 

Ruto na Odinga, ndio wagombea wakuu wa Uchaguzi wa urais nchini Kenya. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.