Pata taarifa kuu

Mombasa: Vita vya maneno vyaibuka kati ya wagombea wakuu kuelekea uchaguzi Kenya

Nchini Kenya, kampeni zinamalizika kesho kuelekea uchaguzi wa wiki ijayo. Leo na jana wagombea wakuu wa urais William Ruto na Raila Odinga, wanawaria wapiga kura huko Mombasa kuwapigia kura, wakiahidi kuimarisha shughuli za bandari, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya ajira kupungua baada ya bandari kavu kujengwa jijini Nairobi na Naivasha na kuzua mivutano ya kisiasa. 

Katika jiji la pwani la Mombasa (Kenya), Februari 11, 2022.
Katika jiji la pwani la Mombasa (Kenya), Februari 11, 2022. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Kinyang'anyiro cha kutafuta kura za Mombasa na Pwani zimesabababisha vita vya maneno kati ya wagombea wakuu wa urais Raila Odinga na William Ruto, wanaomba kura kwa wakazi wa mji huo kwa ahadi ya kuboresha shughuli katika bandari hiyo inayosalia kitega uchumi kikubwa kwa wakaazi wa Mombasa. 

Katika kampeni zake mjii Mombasa, Odinga amekuwa akitoa ahadi hii. 

"Tunajua yale ambaye yanaitwa kufufua bandari hapa, pili vilevile mambo ya Dongo Kundu tunajua. Mimi ndio nilipanga mambo ya Dongo Kundu. Mimi nikienda pale nitatekeleza mara moja." 

Ruto naye  katika kampeni zake amekuwa akisema  mojawapo ya sera zake ni kuhakikisha shughuli za bandari hazitatatizwa. 

"Tumeketi chini tumeweka sahihi mkataba kwamba tarehe 10 Agosti, tukimaliza mambo ya uchaguzi ile shughuli ya bandari ambayo imepelekwa kule Naivasha na Nairobi, ikafanya vijana wa Mombasa karibu elfu saba wakose ajira, na ikafanya Mombasa ikawa kama ni mahame, inarudi hapa Pwani kwa sababu hiyo ni haki ya watu wa Pwani.) 

Abdulswamad Shariff Nassir anawania Ugavana wa Mombasa, amesema "baba lazima mambo ya bandari, hawa mafisadi walivyofanya, bandari yetu tunataka ireje kwa watu wa Mombasa.) 

Mwenyekiti kutoka mwamvuli wa Fast Action Movement,  Salim Karama, ametoa ujumbe huu kwa wagombea hao. 

"Neno kubwa kwa sasa Kenya nzima wanatumia ama wakija Mombasa wanatumia suala la bandari na bado ukiritimba na ulazimizaji bado unaendelea. Ubinafsishaji ule ni haramu, tuna mikakati ya kupambana na dhuluma hizi kupitia kwa njia na taasisi zote za kisheria." 

Bandari ya Mombasa imesalia eneo muhimu kwa uchumi wa watu Pwani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.