Pata taarifa kuu
Kenya - Siasa

Kenya : Hatutasusia uchaguzi asema Raila Odinga

Mgombea urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, nchini Kenya,  Raila Odinga amesema hawawezi kususia uchaguzi wa mwezi ujao, huku akisema ana imani kubwa ya kuibuka mshindi, siku moja baada ya kuitaka tume ya uchaguzi kutumia madaftari ya kieletoniki na lile la  kitabu kuwatambua wapiga kura.

Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga
Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga © Raila Odinga twitter
Matangazo ya kibiashara

Kauli yake inajiri siku chache baada yake kutishia kuwa huenda uchaguzi hautafanyika iwapo tume ya uchaguzi, IEBC,  hatatumia daftari la kitabu kuwatambua wapiga kura, Odinga akisema wito wake ulilenga kuhakikisha tume ya uchaguzi inaandaa uchaguzi wa huru na haki.

Odinga amesema muungano wake hauogopi uchaguzi na kwamba ana imani wataibuka washindi huku akitaka serikali kuhakikisha uchaguzi huo utakuwa wa huru na haki kwa mjibu wa sheria.

Raila anashikiza kutumika kwa sajili ya wapiga kura ya daftari na ile ya kielectronik akisema hilo litahakikisha kila mkenya mpiga kura anapata nafasi ya kupiga kura, iwapo jina lake hatambuliwa kwenye mfumo wa electronik, huku tume ya uchaguzi IEBC, ikisisitiza kuwa itatumia mfumo wa electronik pekee kuwatambua wapiga kura.

Kwa upande wake mgombea urais kupitia muungano wa Kenya Kwanza, naibu rais wa taifa hilo William Ruto, anamtaka Odinga kukoma kuitisha tume ya uchaguzi, wakati huo Kenya Kwanza ikiwa tayari imeunga mkono matumizi ya mfumo wa electonik kuwatambua wapiga kura.

Hata hivyo tume ya Uchaguzi ambayo ambayo tayari imeanza kupokea makaratasi ya kupigia kura, yanayochapishwa nchini Ugiriki, imewahakikishia wakenya kuwa, uchaguzi wa tarehe 9 Agosti, utakuwa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.