Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Wagombea wakuu wanaowania urais nchini Kenya waweka wazi mipango yao

Nchini Kenya, wagombea wakuu naibu rais William Ruto na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, wanaotafuta urais wakati wa uchaguzi Mkuu mwezi ujao, sasa wameweka wazi mipango yao, watakayotekeleza iwapo mmoja wao ataingia Ikulu.

Mabango ya wagombea urais nchini Kenya Raila Odinga na William Ruto jijini Nairobi
Mabango ya wagombea urais nchini Kenya Raila Odinga na William Ruto jijini Nairobi AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

William Ruto anayewania urais kupitia muungano siasa wa Kenya Kwanza, jana usiku alizundia ilani yake jana jioni, amekuja na mambo matoni kikukubwa akiahidi kuongoza mapinduzi ya kiuchumi iwapo ataunda serikali.

Ruto ameahidi kutoa mabilioni ya fedha za Kenya, kuimarisha sekta ya Kilimo anayosema ni tegemeo kubwa la ukuaji wa uchumi nchini humo, lakini pia atatoa mikopo kwa makundi ya vijana, kujiajiri.

Raila Odinga ambaye pia aliweka wazi mipango yake  10 wiki kadhaa zilizopita aliahidi kuwalenga vijana katika mpango wake wa kiuchumi, naye akiajhidi kutoa mkopo kwa vijana na kuwapa muda wa hadi miaka saba, ili kuurejesha mkopo huo bila faida na kuanzisha mpango wa kuwapa masikini Shilingi za nchi hiyo Elfu sita kila mwezi.

Aidha, Ruto ameahidi kuhakikishia kuwa kima família ina bima ya afya ambayo itatumiwa kwa pamoja, huku Odinga naye akiahidi kumpa kila mwananchi bima ya afya chini ya mfumo utakaoitwa BABA Care.

Wachambuzi wa siasa wanasema pamoja na kwamba ilani ya Ruto ilikuwa na uchambuzi wa kina, swali kubwa ni iwapo itatekeleza iwapo ataingia madarakani, swali hili pia linaulizwa kwa ahadi alizotoa Odinga.

Aidha, wadadisi wa siasa za nchi hiyo wanaona kuwa, hatua ya wagombea hao kueleza mipango yao hakutabadilisha kwa kiasi kikubwa wapiga kura nchini humo ambao wameshaamua ni nani watampigia kura, kwa sababu siasa zimetawaliwa na ukanda na ukabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.