Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Volodymyr Zelensky kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atapanda jukwaani katika ukumbi wa Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza leo Jumanne, na kuhutubia viongozi dunia iliogawanyika na kutikiswa na migogoro ya mfululizo, hasa uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi yake.

Kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York mnamo Oktoba 12, 2022
Kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York mnamo Oktoba 12, 2022 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwaka mmoja uliopita, aliidhinishwa kwa hali ya kipekee kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wa video. Wakati huu, atakuwa atashiriki mkutano huo wa ngazi ya juu wa kila mwaka siku ya Jumanne na mkutano maalum wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, kabla ya kuondoka kuelekea Washington ambako atapokelewa katika Ikulu ya Marekani siku Alhamisi.

"Kwetu sisi, ni muhimu sana maneno yetu, jumbe zetu zote, zisikike na washirika wetu," alisema siku ya Jumatatu wakati akikutana na wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa katika hospitali ya New York.

'Pendekezo halisi' litawasilishwa

"Ukraine itawasilisha pendekezo halisi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kuimarisha kanuni ya uadilifu wa eneo na kuboresha uwezo wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia na kukomesha uvamizi," alisema.

Tangu uvamizi wa Urusi, nchi nyingi zimepitisha maazimio kadhaa katika Mkutano Muu wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono Ukraine na ukamilifu wa eneo lake au kutaka Urusi iondoke nchini Ukraine.

Lakini baada ya mwaka mmoja na nusu wa vita na madhara makubwa duniani, hasa katika usalama wa chakula, baadhi ya nchi za Kusini zinaomba suluhu la kidiplomasia.

"Ninafahamu kwamba kwa baadhi ya viongozi, ni muhimu kupata suluhisho la amani," alibainisha Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel. Lakini "ili amani hii idumu, ni lazima iheshimu kanuni" za Umoja wa Mataifa, alikasirisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.