Pata taarifa kuu

Tabia nchi: Julai 2023 ndio mwezi wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa Duniani

Mwezi Julai 2023 utakuwa mwezi wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa duniani. Hayo yamebainishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO, na taasisi ya Ulaya ya Copernicus mnamo Alhamisi Julai 27. Hali ambayo, bila ya kushangaza, inakwenda sambamba katika mwelekeo wa utabiri wa wataalamu wa hali ya hewa.

Joto kali lililoikumba Ugiriki mnamo mwezi Julai 2023 linaweka viumbe mbalimbali kwenye mtihani. Huko Athens, juu ya kilima cha Acropolis, mgeni anatatizika kustahimili halijoto ya tarehe 14 Julai 2023.
Joto kali lililoikumba Ugiriki mnamo mwezi Julai 2023 linaweka viumbe mbalimbali kwenye mtihani. Huko Athens, juu ya kilima cha Acropolis, mgeni anatatizika kustahimili halijoto ya tarehe 14 Julai 2023. REUTERS - LOUIZA VRADI
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mwezi wa Juni 2023 ambao tayari umekuwa na rekodi, mwezi huu wa Julai 2023 utakuwa na joto zaidi kuwahi kurekodiwa. Hali ya joto isiyo ya kawaida kiasi kwamba si lazima kusubiri hadi mwisho wa mwezi ili kuthibitisha rekodi: katika miaka 100,000 iliyopita, Dunia haijawahi kushuhudia mwezi wa joto kama huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amebaini kwamba tumehama kutoka enzi ya ongezeko la joto hadi "zama za hali kuchemka". Na anaongeza kwamba huu ni mwanzo tu, hata kama, kwa wanasayansi, bado kuna wakati wa kuchukua hatua.

Kulingana na Taasisi ya Copernicus, hakuna uwezekano kwamba rekodi hii ya mwezi wa Julai itabaki hivyo mwaka huu bila kuleta madhara, hasa na kuongezeka kwa nguvu kwa wa hali ya asili ya mfumo wa hali ya hewa El Nino, sawa na ongezeko la joto duniani. Lakini binadamu ndiye anayehusika zaidi na halijoto hizi za kipekee zilizorekodiwa kila duniani. Uzalishaji wa gesi chafu unaendelea kudhuru hali ya hewa.

Huku hali ya hewa duniani sasa ikizunguka karibu 1.2°C ya ongezeko la joto, lengo la Mkataba wa Paris la kutozidisha 1.5°C linaonekana kuwa gumu kuafikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.