Pata taarifa kuu

Kuisaidia Ukraine kutaimarisha uchumi wa dunia : Janet Yellen

Nairobi – Kuongeza kasi kuisaidia nchi ya Ukraine ‘ni moja ya suluhu’ ya kujenga uchumi wa dunia, amesema waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen, kando ya mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka muungano wa nchi za G20 unaofanyika India.

Waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen
Waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen REUTERS - SARAH SILBIGER
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wake na wadau, Yellen ametupilia mbali madai kuwa Jumuiya ya kimataifa imejikita zaidi kuisaidia Ukraine na kuziacha nchi zinazoendelea.

Kuimaliza vita ya Ukraine, kunapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza cha mataifa yenye nguvu, amesema waziri Yellen, ambapo akaongeza kuwa kuisaidia nchi hiyo kifedha kutasaidia kuimarisha uchumi wa dunia.

Aidha, Yellen ameonya kuhusu kasi ndogo ya kushughulikia changamoto za madeni kwa nchi masikini pamoja na mabadiliko katika taasisi za kifedha, akisema ni mapema sana kufikiria kuondoa vikwazo vya kikodi kwa nchi ya China.

Hata hivyo wataalamu wamekosoa mkutano wa G20 kufanyika India, taifa ambalo hadi sasa halijakashifu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.