Pata taarifa kuu

Erdogan: Mkataba wa nafaka kutoka Ukraine waongezwa kwa miezi miwili

NAIROBI – Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumatano ametangaza kuongeza kwa miezi miwili, mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa Ukraine kusafirisha nafaka kupitia Black Sea.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan AP - Turkish Presidency
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Uturuki ametoa tangazo hilo, siku moja kabla ya makataa ya mpango huo kukamilika, na kujipatia alama wakati huu uchaguzi wa urais ukitarajiwa kufanyika Mei 28 ambapo anawania muhula mwingine.

Erdogan kwenye hotuba yake kupitia runinga nchini mwake, amewashukuru rais wa Urusi Vladimir Putin, mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa kuongeza muda huo.

Ukraine ni mzalishaji na muuzaji mkubwa wa nafaka, kabla ya uvamizi wa Urusi mnamo Februari mwaka 2022, ambapo meli za kivita za Urusi ziliziba bandari za Bahari Nyeusi za Ukraine, na hivyo kupelekea bei ya vyakula kupanda katika masoko ya kimataifa na kuwakumba watu maskini zaidi duniani.

Mkataba wa kwanza kati ya Uturuki na Umoja wa Mataifa ulifikiwa Julai 2022, na ndio pekee ambao umesainiwa na mataifa ya Urusi na Ukraine tangu kuanza kwa vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.