Pata taarifa kuu

Biden kukutana na viongozi wa Pasifiki huko Papua New Guinea

NAIROBI – Rais wa Marekani, Joe Biden, atakutana na viongozi 18 kutoka Pasifiki ya Kusini, wakati atakapozuru Papua New Guinea mwezi Mei.

Rais wa Marekani Joe Biden, huko Washington, Machi 27, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden, huko Washington, Machi 27, 2023. AP - Alex Brandon
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa Aprili 29, na ofisa mkuu wa eneo hilo, inakuja katika kipindi hiki ambapo Marekani na China zinajipima nguvu kuhusu nani ndio mshawishi mkuu katika eneo hilo.

Eneo la Pasifiki ya Kusini lilionekana kuwa sehemu ya kidiplomasia baada ya vita vya pili vya dunia, lakini linazidi kuwa uwanja wa mataifa yenye nguvu kupimana ushawishi katika nyanja za kibiashara, kisiasa na kijeshi.

Waziri wa mambo ya nje wa Papua New Guinea, Justin Tkatchenko, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba Biden kadhalika atahudhuria mazungumzo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Mawaziri wakuu wa nchi za Australia na New Zealand, watahudhuria mkutano wa wanachama 18 wa Visiwa vya Pasifiki, yanayojumuisha maeneo madogo, yaliyotawanyika katika eneo kubwa la bahari.

Biden atakuwa rais wa Marekani ambaye yuko madarakani kuzuru Papua New Guinea mnamo Mei 22. Biden pia ameratibiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7 huko Hiroshima, Japan, na mkutano wa kilele wa Quad huko Sydney mwezi ujao, ambao unajumuisha mataifa ya Australia, India, Japan na Marekani.

Ubabe wa China na Marekani

Mjumbe maalum wa Marekani Joseph Yun, amesema wiki hii kwamba Marekani ilikuwa inajituma kuongeza ushawishi wake baada ya miaka mingi ya kupuuzwa ambapo ushawishi wa China uliongezeka katika Pasifiki ya Kusini.

Hivi majuzi, China ilitia saini mkataba wa siri wa usalama na Visiwa vya Solomon, mashariki mwa Papua New Guinea, ambao unaweza kuruhusu wanajeshi wa China kutumwa au kuweka makao huko.

Ni ukanda ambayo inaweza kuwa muhimu katika machafuko yoyote ya kijeshi yanayowezekana juu ya Taiwan.

Safari hii ya Biden pia inaweza kuhitimisha mkataba wa ushirikiano wa ulinzi wa Marekani na Papua New Guinea, ambao utaruhusu mafunzo zaidi ya pamoja na maendeleo ya miundombinu ya usalama.

Washington inafanya kazi ya kuanzisha kituo cha pamoja cha wanamaji huko Lombrum kwenye Kisiwa cha Manus cha Papua New Guinea, ujenzi ulioanza katikati ya 2020, kulingana na Idara ya Ulinzi ya Australia, ambayo pia inashiriki katika mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.