Pata taarifa kuu

UN: Mabadiliko ya hali ya hewa yanachochea biashara haramu ya binadamu

Mabadiliko ya hali ya hewa yanazidisha biashara haramu ya binadamu duniani kote. Hili ni hitimisho la ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) iliyochapishwa Jumanne, Januari 23.

Watu walionusurika na Kimbunga Haiyan, huko Tacloban, Ufilipino, mwaka wa 2013.
Watu walionusurika na Kimbunga Haiyan, huko Tacloban, Ufilipino, mwaka wa 2013. REUTERS/Romeo Ranoco
Matangazo ya kibiashara

UNODC inazingatia data zilizokusanywa katika nchi 141 katika kipindi cha 2017-2020 na uchanganuzi wa kesi 800 za mahakama. Kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa, ambayo huwasukuma mamilioni ya watu barabarani, leo hii ni mojawapo ya "sababu kuu" za biashara haramu ya binadamu.

Nchini Ufilipino, kwa mfano, biashara haramu ya binadamu iliongezeka baada ya kimbunga cha Haiyan cha mwaka wa 2013.

Baada ya muda, "maeneo yote yatakuwa hayaweza tena kukaliwa na watu", hali ambayo "inaathiri vibaya" jamii maskini zinazoishi hasa kutokana na kilimo au uvuvi. Wanajikuta "wananyimwa uwezo wao wa kujikimu kimaisha na kulazimishwa kutoroka jamii zao", na hivyo kuwa mawindo rahisi kwa wafanyabiashara, ameelezea Fabrizio Sarrica, mwandishi mkuu wa ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inataja vimbunga vikali nchini Ufilipino, au hata Bangladesh, ambayo huathiriwa hasa na vimbunga na dhoruba. Katika nchi zote mbili, ongezeko la visa vya usafirishaji haramu wa binadamu limeonekana, kwa mfano, kuandaliwa kwa "kampeni kubwa za kuajiri" ili kuwanasa maskini zaidi katika kazi ya kulazimishwa.

"Baada ya kimbunga nchini Ufilipino, mamlaka ya kitaifa iligundua idadi kubwa ya waathiriwa wa ulanguzi. Idadi ya kipekee ikilinganishwa na miaka iliyopita, anasisitiza Giulia Serio, mtaalamu wa UNODC. Uchambuzi wetu unaangalia jinsi watu walioathiriwa walilazimika kufanya chaguzi ngumu sana ili kupata kukidhi maisha na kutafuta uwezo wa kijamii na kiuchumi katika sehemu zingine za nchi. Na katika hali hii, walijikuta wakikabiliwa na uhalifu wa kusafirisha watu. Kesi inayohusu Ufilipino, kwa mfano, ni kesi ya wanawake ambao wanatumikishwa kama wafanyakazi wa nyumbani, ambao wanaajiriwa nchini Ufilipino na kisha kutumwa katika nchi zingine ambapo lazima wafanye kazi za nyumbani, ambapo wanaweza kulazimishwa kufanya vya aibu, ukahaba au ngono.”

Vita na Uviko-19

Ghana, mwathirika wa ukame na mafuriko, na eneo la Karibi, lililo chini ya vimbunga na kupanda kwa kina cha bahari, pia ziko mstari wa mbele.

Mazalia mengine ya biashara haramu ni migogoro ya kivita. Ikiwa Afrika ndilo bara lililoathiriwa zaidi, shirika la Umoja wa Mataifa linaashiria hali inayoweza kuwa "hatari" nchini Ukraine, huku ikikaribisha hatua zilizochukuliwa na nchi za Umoja wa Ulaya kukaribisha na kulinda mamilioni ya wakimbizi.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ukusanyaji wa takwimu, idadi ya waathiriwa waliorekodiwa ilipungua mnamo 2020. Athari za janga la Uviko-19 ambalo lilifanya ugunduzi wa kesi usiwe dhahiri. Pamoja na kufungwa kwa maeneo yaliyo wazi kwa umma (baa, vilabu vya usiku, n.k.) kwa sababu ya vikwazo vya afya, aina fulani za ulanguzi, hasa unyanyasaji wa kijinsia, zimehamia "sehemu zisizoonekana sana na hata zisizo salama".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.