Pata taarifa kuu
DUNIA-UKIMWI

Dunia yaadhimisha siku ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi

Dunia, inaadhimisha  siku ya kupambana na maambukizi ya virusi vya  Ukimwi duniani, wazo kuu la mwaka 2022 likiwa ni kusawazisha kwa lengo la kuhimiza dunia, kuchukua hatua za kusitisha maambukizi mapya.

Nembo ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi
Nembo ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi Getty Images/iStockphoto - Surasak Taykeaw
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na upambanaji wa ugonjwa huo UNAIDS linasema kuna umuhimu wa kuongeza matibabu kwa walioambukizwa, kufanya vipimo na kuendelea kutoa elimu ya kuzuia maambukizi mapya.

Aidha, watalaam wa afya wanasema, mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi bado ni changamoto kubwa katika jamii licha ya hatua kupigwa katika miaka kadhaa iliyopita.

Miongoni mwa changamoto zinazokwamisha vita dhidi ya ugonjwa huo duniani, ni pamoja na mataifa ya dunia, kutotekeleza ahadi za kutoa fedha kusaidia katika mapambano hayo na hivyo kuhatarisha maisha ya mamilioni ya watu.

Mgawanyiko na kutoheshimiwa kwa haki za binadamu, ni miongoni mwa mambo ambayo yamesababisha ugonjwa huu kusalia janga la dunia.

Kila tarehe   Disemba tangu, mwaka 1988, siku hii ilitengwa ili kuwahamasisha watu kuhusu namna ugonjwa huu unavyoambukizwa na namna ya kuuzuia, pamoja na kuwaomboleza wale waliopoteza maisha kutokana na maambukizi hayo.

Takwimu muhimu

Tangu kuanza kwa janga hili, mwaka 1981, watu Milioni  84.2 wameambukizwa na wengine Milioni 40.1 wamepoteza maisha tangu kugundulika kwa ugonjwa huu Juni, 5 1981.

Hadi mwaka mmoja uliopita wa 2021, watu Milioni 38.4 wanaishi na maambukizi ya Ukimwi duniani.

Watu wengine Milion 1.5 waliambukizwa virusi hivyo mwaka 2021 pekee.

Watu 650 000, walifariki dunia kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.