Pata taarifa kuu

COP27: Majadiliano ya dakika za mwisho kujaribu kupata makubaliano

Labda siku ya mwisho ya COP27 huko Sharm el-Sheikh (Misri), Jumamosi hii Novemba 19, lakini bado hakuna makubaliano juu ya masuala magumu yanayohusu njia za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Rasimu ya makubaliano ya hivi punde iliwekwa hadharani jana asubuhi. Na tangu wakati huo, kufikia sasa hakuna makubaliano yoyote ambayo yamefikiwa. Mazungumzo yanaendelea na ni magumu.

Licha ya hotuba ya Joe Biden mnamo Novemba 11 katika mkutano wa Tabia nchi (COP27) (picha yetu), mazungumzo ya mwisho yameshindikana na ni magumu. Zaidi ya hayo, Marekani imesalia nyuma sana kwenye majadiliano katika siku za hivi karibuni.
Licha ya hotuba ya Joe Biden mnamo Novemba 11 katika mkutano wa Tabia nchi (COP27) (picha yetu), mazungumzo ya mwisho yameshindikana na ni magumu. Zaidi ya hayo, Marekani imesalia nyuma sana kwenye majadiliano katika siku za hivi karibuni. AFP - AHMAD GHARABLI
Matangazo ya kibiashara

 

Katika mkutano wa kimataifa wa Mazingira, COP27, huko Sharm el-Sheikh, washiriki sio wengi kama ulivyoanza, maduka ya kahawa yamevunjwa. Na wajumbe wanaanza kuondoka. Kmekuwa na ukimya asubuhi ya leo Jumamosi katika makao makuu ya Bunge ambapo kunafanyika mkutano huo, baada ya wiki yenye shughuli nyingi ambapo makumi kadhaa ya maelfu ya watu walisajiliwa. Tangu Ijumaa, Novemba 18, hakuna mapendekezo ya makubaliano mapya. Nakala mpya ilitarajiwa siku ya Ijumaa mchana, kisha usiku lakini bado hakuna chochote kimefikiwa.

Mkutano huo wa wiki mbili unaofanyika mjini Sharm el-Sheikh ulitarajiwa kumalizika jana Ijumaa lakini ukapelekwa mbele hadi leo kwa matumaini ya kufikia makubaliano hayo.

Jinsi ya kupata maelewano?

Kwa uhakika maswali yameibuka juu ya uwezekano wa kupata makubaliano katika saa zijazo. Aurore Mathieu ni afisaa wa kisiasa wa kimataifa wa Mtandao wa Hatua za Tabia nchi: “Ndiyo, tunaweza kuondoka bila makubaliano. Nchi zimegawanyika katika msimamo wao hivi sasa. Kweli kuna dau kubwa la kisiasa kwa nchi za Kusini kuondoka na utaratibu huu wa kifedha ambao bado hawakuwa nao mwaka jana na ambao wanataka wanufaike. Umoja wa Ulaya, una hisia ya kuwa tayari umefanya kiwango cha juu. Kwa hivyo tuko pamoja na Marekani, ambayo kwa sasa haijajiweka sawa. Kwa hivyo, inawezekana kwamba kila nchi itarudi nyumbani bila kuwa na makubaliano katika mkutano huu wa Tabia nchio (COP27)”.

Marekani yasalia nyuma

Jana kuna taarifa ambayo imebaini kwamba mjumbe wa Marekani John Kerry alipimwa na kukutwa liambukizwa UVIKO-19. Hii haitarahisisha kipindi cha mwisho cha mazungumzo hayo, huku mengi yakitarajiwa kutoka upande wa Marekani ambayo imesalia nyuma sana katika siku za hivi karibuni.

Kwa hivyo, mambo ambayo bado yamezuiliwa: swali la utaratibu huu mpya wa ufadhili wa "hasara na uharibifu", lengo la kudumisha ongezeko la joto duniani kwa 1.5 ° kama ilivyorekodiwa na makubaliano ya Paris.

Suala llinaloleta mvutano ni la fidia ya fedha kwa uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya Tabia nchi katika mataifa masikini duniani. Mataifa yanayoendelea yamekuwa yakisisitiza fidia hiyo kwa mataifa masikini yanayoathirika na mabadiliko ya Tabia nchi jambo ambalo nchi tajiri zimekataa kuridhia kwa muda sasa. Hata hivyo Umoja wa Ulaya umeonyesha dalili ya kukubali hilo lakini kwa masharti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.