Pata taarifa kuu
AFYA YA PAPA FRANCIS

Afya ya papa: Naweza jiuzulu – japokuwa muda bado, papa Francis

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, ametangaza kuwa muda unakaribia ambapo anaweza wazia swala la kujiuzulu na atafanya hivyo iwapo atashawishika kuwa afya yake haimruhusu kuendelea kuhudumu anavyotakiwa.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani -Papa Francis Juni  27  2022.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani -Papa Francis Juni 27 2022. © AP - Alessandra Tarantino
Matangazo ya kibiashara

Papa amezungumzia swala hili wakati akihitimisha ziara yake nchini Canada,ambako aliwaomba msamaha walizwa wa nchini humo, ziara ambayo ilimlazimu kusafiri kwa muda mrefu.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85, licha ya kugusia swala la kustaafu, amesisitiza kuwa kwa sasa ataendelea kutekeleza majukumu yake na ataongozwa na Mungu kuhusu wakati wake wa kujiuzulu ukifika.

Kwa miezi sasa Papa Francis amekuwa akiuumwa na goti hali ambayo imempa matatizo ya kutembea. Akiwa nchini Canada,ametumia muda mwingi kutembea akitumia kiti cha magurudumu.

Licha ya kuumbwa na tatizo la goti, kiongozi huyo amepuuzia mbali madi kuwa huenda akawa anakumbwa na changamoto zengine hatari za kiafya.

Mwaka wa 2013, Papa Benedict XI, mtangulizi wake Papa Francis, alijiuzulu kabla ya muda wake kufika kutokana na changamoto za kiafya.

Aidha kiongozi huyo ameeleza kuwa anawazia kufanya ziara nchini Ukraine hivi karibuni japokuwa atasikiliza ushauri wa madktari wake kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.