Pata taarifa kuu
DUNIA- AFYA

UN: Vita dhidi ya maambukizi ya ukimwi duniani vimo hatarani

Vita dhidi ya maambukizi ya ukimwi duniani vimeripotiwa kuathirika pakubwa kutokana na uwepo wa janaga la uviko 19 pamoja na changamoto nyengine zinazoikumba dunia.

Mhudumu wa afya akiwa na dawa za kupigana na maambukizi ya ukimwi
Mhudumu wa afya akiwa na dawa za kupigana na maambukizi ya ukimwi www.unaids.org
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii imewasilishwa katika kongamano kuhusu ukimwi duniani jijini Montreal nchini Canada inaeleza kuwa kiwango kikubwa cha fedha zilizokuwa zimetengewa vita hivyo, zimeripotiwa kuelekezwa katika vita dhidi ya msambao wa uviko 19.

Vita kati ya Ukraine na Urusi vimetajwa pia kuathiri pakubwa juhudi za kabiliana na ukimwi duniani.

Ripoti hiyo ya UNAIDS, inaonyesha kuwa maambukizi ya ukimwi duniani yameshuka kwa asilimia 3.6 kati ya mwaka wa 2020 na 2021, idadi ambayo ni ndogo zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka wa 2016.

Mwaka jana peke, maambukizi mapya milioni 1.5 yaliripotiwa, idadi ambayo ilipita viwango katika mapambano dhidi ya ukimwi duniani.

Maambukizi mapya ya ukimwi yameripotiwa kuongezeka kaskazini mwa ya Bara Europa, katikati ya Bara Asia, mashariki ya kati na Afrika kaskazini.

Karibia watu milioni 38.4 duniani walikuwa wameambukizwa ukimwi mwaka wa 2021, watu wengine zaidi ya laki sita wakiripotiwa kufariki kutokana na maambukizi ya ukimwi.

Rasilimali za kupigana na ukimwi ulimwenguni zilipuungua kwa asilimia 6 mwaka wa 2021, Mchango wa Marekani amabye ni muhusika mkubwa katika vita hivi ukishuka kwa asilimia 57.

Umoja wa mataifa katika ripoti yake unasema kuwa fedha zilizotegewa mataifa yanayoendelea duniani kupigana na ukimwi ni pauni bilioni 8 idadi ambayo ni ndogo zaidi kulingana na inavyohitajika kufikia mwaka wa 2025.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.