Pata taarifa kuu
UN-USALAMA.

Idadi ya watu duniani imefikia watu bilioni 8 mwaka huu: UN

Ripoti ya umoja wa mataifa UN, inaeleza kuwa idadi ya watu wanaoishi duniani inatarajiwa kufikia watu bilioni nane ifikapo tarehe 15 ya mwezi Novemba, UN ikisema kuwa India itaipiku China katika orodha ya mataifa yalio na watu wengi ulimwenguni ifikapo mwaka wa 2023.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ,Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ,Antonio Guterres AP - Theresa Wey
Matangazo ya kibiashara

Utafiti huo uliofanywa na kitengo cha maswala ya kiuchumi katika umoja wa mataifa imeonyesha kuwa idadi ya watu ulimwenguni imekuwa ikiongezeka kwa kasi ya chini tangu mwaka wa 1950.

Aidha UN inaeleza kuwa idadi hiyo ya watu duniani inatarajiwa kufikia watu bilioni 8.5 katika mwaka wa 2030 kabla ya kupanda na kufikia idadi ya watu bilioni 9.7 kuelekea mwaka wa 2050.

Idadi hiyo vile vile inatarajiwa kufikia watu bilioni 10.4 katika miaka ya 2080.

Japokuwa idadi ya watoto wanaozaliwa katika mataifa yanaoyoendelea imeripotiwa kushuka, takwimu hizo zinatarajiwa kupanda katika kipindi cha miaka ijayo katika mataifa manane ya uliwenguni.

Mataifa hayo yanayotarajiwa kushuhudia ongezeko la idadi ya watoto wanaozaliwa kulingana na utafiti huo wa UN ni pamoja na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Misiri, Ethiopia, India, Nigeria, Pakistan, Ufilipino na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.