Pata taarifa kuu

Wakristo washerehekea siku ya kuzaliwa kwa mwokozi wao Yesu Kristo

Wakiristo kote duniani, wanasherehekea sikukuu ya Krismasi, siku wanayoamini, mwokozi wao Yesu Kristo alizaliwa. Hata hivyo, kwa mwaka wa pili sasa, siku hii inaadhimishwa kwenye mazingira magumu, kufuatia ulimwengu kuendelea kusumbuliwa na janga la Covid-19.

Papa Francis kwenye akihutubia Waksisto katika kanisa la Mtakatifu Peter huko Roma wakati maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Yesu Kristo mnamo Desemba 25, 2021.
Papa Francis kwenye akihutubia Waksisto katika kanisa la Mtakatifu Peter huko Roma wakati maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Yesu Kristo mnamo Desemba 25, 2021. AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Mabilioni ya watu wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi, wakati huu serikali mbalimbali zikitangaza masharti ya kupambana na janga la Covid-19, hasa wakati huu kirusi koipya cha omicron kinapoendelea kusambaa kwa kasi.

Kinyume na miaka iliyopita, watu katika nchi mbalimbali waliojumuika katika nyumba za ibada na maeneo ya burudani, walivalia barakoa na kukaa kwa umbali wa mita moja ili kuzuia maambukizi.

Mjini Vatican, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, aliongoza misa ya watu karibu Elfu mbili, wote waliokuwa wamevalia barakoa, na kutoa wito wa amani na upendo duniani.

Nchini Israel, anakoaminiwa alizaliwa Yesu katika mji wa Bethlehem, watalii kutoka nje ya nchi hawakuruhusiwa kuzueu êneo hilo baada ya serikali kufunga mipaka kwa sababu ya maambukizi ya kirusi cha omicron.

Nchini Marekani, mamilioni ya watu wameonekana wakisafiri kwenda kukutana na ndugu zao licha maambukizi kuongezeka.

Barani Afrika, hasa katika mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Wakiristo waliamkia Makanisani na baadaye kwenda kwenda kutalii katika maeneo mbalimbali huku serikali za nchi zao zikiendelea kuwahimiza watu Wake, kusherehekea kwa uangalifu, kwa kuhakikisha wanavaa barakoa, kukaa kwa umbali, kunawa mikono na kupata chanjo ili kupambana na maambukizi ya Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.