Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Shughuli katika kiwanda cha JBS zazorota baada ya shambulio la kimtandao

Kiwanda kikubwa cha kusindika nyama duniani, cha JBS  kimeshambuliwa na wahalifu wa mtandaoni, na kusababisha shughuli za kila siku kutatitiza.

Kiwanda cha nyama za nguruwe cha JBS huko Worthington, Minnesota, Marekani.
Kiwanda cha nyama za nguruwe cha JBS huko Worthington, Minnesota, Marekani. REUTERS - Bing Guan
Matangazo ya kibiashara

Tarakishi kwenye kiwanda hicho nchini Australia, Canada na Marekani zimeshambuliwa na wahalifu hao wa mtandaoni na kukwamisha kazi.

Kampuni hiyo imefunga kwa muda katika nchi hizo, huku maelfu ya wafanyakazi wakishidwa kuendelea na kazi.

Marekani inamaani kuwa, uvamizi huo umetokea nchini Urusi kwa mujibu wa ripoti kutoka Ikulu ya White House ambayo imesema uchunguzi zaidi unaendelea.

Shamnbulizi hili la mtandao linamaanisha kuwa nchi hizo zitashuhudia uhaba wa nyama lakini pia bei itapanda.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, katika shambulizi kama hili, wavamizi hutishia kuifuta taarifa muhimu iwapo walengwa watashindwa kulipa kikombozi.

Mwezi uliopita, kuliripotiwa tena shambulizi la mtandao katika kampuni kubwa ya mafuta nchini Marekani ambayo ilizamika kulipa kikombozo cha Dola Milioni 4.4 kwa wavamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.