Pata taarifa kuu
DUNIA-COVID 19

Watu Milioni tatu sasa wapoteza maisha kufuatia maambukizi ya Corona dunia

Idadi ya watu waliopoteza maisha duniani, kutokana na maambukizi ya Covid 19 imefikia Milioni tatu kwa mujibu wa takwimu kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.

Mgonjwa wa maambukizi ya Covid 19
Mgonjwa wa maambukizi ya Covid 19 AP - Eraldo Peres
Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo imeongezeka wakati huu nchi mbalimbali duniani zikiendelea kutoa chanjo kwa wananchi wake, huku visa vya maambukizi vikiendelea kuongezeka nchini Brazil, India na Ufaransa.

Mpaka sasa idadi ya watu waliopoteza maisha ni sawa na idadi ya watu kwenye miji ya Kyiev nchini Ukraine na Caracas nchini Venezuela.

Takwimu kutoka chuo Kikuu cha Johns Hopkins, zinaonesha kuwa kila siku watu 12,000 hupoteza maisha kila siku duniani, huku wnegine zaidi ya 700,000 wakiambukizwa.

Nchini Brazil watu karibu 3,000 hupoteza maisha kila siku wakati huu rais wa nchi hiyo akiendelea kushtumiwa kwa kutochokua hatua za makusudi kushinda janga hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.