Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND-AUSTRALIA

Vita vya maeneo vyaibuka kati ya New Zealand na Australia juu ya mwanamke anayezuiliwa Uturuki

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameishtumu Australia kwa kuchukuwa hatua ya kumvua uraia wake mwanamke anayezuiliwa nchini Uturuki bila kuishirikisha na kumshtumu mwanamke huyo kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

Jacinda Ardern, Waziri Mkuu wa New Zealand
Jacinda Ardern, Waziri Mkuu wa New Zealand AAP Image/David Rowland via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii mamlaka nchini Uturuki ilitangaza kuwa imewakamata watu watatu, raia wa New Zealand, watoto wawili na mwanamke mmoja wa miaka 26 anayeshukiwa kuwa mwanachama wa kundi la Islamic State, wakati walipokuwa wakijaribu kuingia nchini kinyume cha sheria kutoka Syria.

Mwanamke huyo alikuwa na uraia pacha wa New Zealand na Australia, lakini serikali ya Australia ilimvua uraia wake, Jacinda Ardern amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Waziri Mkuu wa New Zealand anaona kwamba Australia "imeshindwa kutekeleza majukumu yake" kwa kumvua uraia wake mwanamke huyo bila kushauriana na New Zealand.

New Zealand kwa hivyo inalazimika kuchukua jukumu la kumpokea mwanamke huyu ambaye hajaishi nchini humo tangu akiwa na umri wa miaka sita.

"Kusema ukweli, New Zealand imechoshwa na Australia kwa tabia zake za kutuletea matatizo yake," amesema Waziri Mkuu wa New Zealand. "Vinginevyo, tutachukua majukumu yetu na ndivyo tunaomba Australia ifanye."

"Kazi yangu ni kuwakilisha masilahi ya Australia. Na kama Waziri Mkuu, lazima nihakikishe usalama wa taifa hili unalindwa vilivyo. Nadhani Waustralia wote watakubaliana nami", amejibu Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.