Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND-COVID 19

Kesi ya kwanza yathibitishwa New Zealand tangu Novemba

New Zealand imerekodi kesi ya kwanza ya raia wake kuambukizwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19 tangu miezi miwili iliyopita.

Kirusi cha Corona kinachoendelea kuisumbua dunia
Kirusi cha Corona kinachoendelea kuisumbua dunia NEXU Science Communication | Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mtu aliyepatikana na kirusi cha aina mpya ya Corona kilichoanzia nchini Afrika Kusini, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 56 ambaye alirudi nchini mnamo Desemba 30, Lakini watu walitangamana naye mpaka sasa wanaonekana kuwa hawana dalili zozote za ugonjwa huo, amesema waziri wa afya, Chris Hipkins.

Aliporudi, alikuwa amewekwa kizuizini kwa muda wa wiki mbili lakini akapimwa hasi mara mbili, alisema. Mamlaka zinachunguza uwezekano kwamba aliambukizwa na mtu mwingine katika kituo cha kutengwa alikokuwa.

Mtu wa mwisho kupatiakana na virusi vya Corona nchini New Zealand alithibitishwa Novemba 18, kulingana na wizara ya Afya.

Australia imeamua kufunga kwa muda " anga yake" na jirani yake, New Zealand. Mtu yeyote anayewasili kutoka New Zealand tangu Januari 14 atalazimika kujiweka karantini hadi atakapopimwa na kuonekana kuwa hana maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.