Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini;Mashambulizi ya makombora dhidi ya Marekani hayataepukika

Korea kaskazini imeonya kuwa matusi ya raisi wa Marekani Donald Trump dhidi ya taifa hilo na kiongozi wake halitaiepusha Marekani na mashambulizi ya makombora.

Waziri wa mambo ya kigeni wa korea Kaskazini  Ri Yong-ho akihutubia katika mkutano wa Umoja wa mataifa
Waziri wa mambo ya kigeni wa korea Kaskazini Ri Yong-ho akihutubia katika mkutano wa Umoja wa mataifa REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea kaskazini Ri Yong Hong amesema hayo jumamosi akihutubia mkutano mkuu wa umoja wa mataifa saa kadhaa baada ya Marekani kurusha ndege zake za kivita jirani na Korea Kaskazini.

Waziri Ri aliuambia mkutano wa UN kuwa Kupitia mapambano ya muda mrefu,sasa korea inakaribia hatua za mwisho za kukamilisha taifa lenye nguvu ya nyuklia,

Hivi karibuni raisi wa Marekani Donald Trump alisema ataiangamiza Korea Kaskazini iikiwa Marekani na washirika wake wakilazimika kujitetea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.