Pata taarifa kuu
AMERIKA-AFYA

Athari za maradhi ya zika zaendelea kuibuliwa

Afisa wa juu wa afya nchini Marekani, amesema kuwa kuna ushahidi wa nguvu kuthibitisha kuwa ugonjwa wa virusi vya Zika, una madhara kwa watoto wadogo wanaozaliwa.

Bango linalopiga vita maradhi ya Zika huko Honduras, Feb 6. 2016.
Bango linalopiga vita maradhi ya Zika huko Honduras, Feb 6. 2016. REUTERS/Jorge Cabrera
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mbele ya jopo la wanasiasa kuelezea mwenendo wa maambukizi ya ugonjwa huo nchini Marekani, Dr Tom Frieden mkuu wa kitengo cha kudhibiti magonjwa, amesema uchunguzi uliofanywa kwa watoto wawili wachanga nchini Brazili waliofariki saa chache baada ya kuzaliwa, umeonesha walipata maambukizi kutoka kwa mama.

Hata hivyo Dr Frieden amewaambia wanasiasa hao kuwa hadi sasa hawajabaini moja kwa moja ikiwa kuna uhusiano mkubwa wa ugonjwa huo na mbu wanaobeba virusi vyenyewe vya Zika.

Amewataka pia wanawake nchini Marekani wanaopanga kusafiri kwenda Brazil na mataifa mengine ya America, kuahirisha safari zao.

Inakadiriwa kuwa kuna watoto zaidi ya elfu 4 nchini Brazil peke yake, ambao wameathiriwa na virusi vya Zika ambavyo husababisha mtoto anayezaliwa kuwa na kichwa na ubongo mdogo na kwamba walipata maambukizi hayo toka kwa mama zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.