Pata taarifa kuu
VATICAN

Salaam za Pasaka:Papa Francis awataka wakristo kueneza ujumbe wa Mungu kwa watu wote

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa wito kwa Wakristo kupeleka ujumbe wa Mungu katika miisho ya dunia wakati wa ibada ya maadhimisho ya Pasaka katika kanisa la mtakatifu Petro jijini Vatikani.  

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis REUTERS/Alessandro Bianchi
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis amesema kuwa msingi wa ujumbe wa Pasaka ni kurudi katika misingi ya imani kwa kutafakari kama umekwenda katika njia iliyokufanya usahau misingi ya Imani.

Amesema kuna haja ya kufufua moto ambao Yesu amewasha katika dunia na kuleta moto huo kwa watu wote,katika miisho ya dunia

Naye Askofu Severine Niwemugizi  wa kanisa katoliki Ngara  Tanzania ametilia mkazo historia ya wokovu wa wanadamu akiwataka wakristo kuutunza moto wa Kristo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.