Pata taarifa kuu
SYRIA-Mazungumzo

Uingereza na Ufaransa zalaumu serikali ya Syria kwa kuzorotesha mazungumzo ya amani ya Geneva

Uingereza na Ufaransa zimeilaumu serikali ya Syria kwa kuzorotesha mazungumzo ya amani kati yao na upinzani huko Geneva.

Mapatanishi wa Mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi
Mapatanishi wa Mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Willium Hague amesema lawama zote zinapaswa kuelekezwa kwa utawala wa Assad huku waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius akisema serikali hiyo imezuia ufanisi wa mazungumzo hayo.

Hali hiyo ilimsukuma Mpatanishi wa mzozo wa syria Lakhdar Brahimi kutaka radhi raia wa Syria kufuatia kumalizika kwa mazungumzo ya Geneva bila kuwa na matumaini ya kutatuliwa kwa mzozo huo.

Kiongozi huyo alikutana katika majadiliano ya mwisho na pande mbili huko geneva kumaliza mzozo uliopo kati ya serikali ya Syria na upinzani nchini humo ambapo hoja ya msingi ilikuwa ni hatua ya serikali kukataa kuzungumzia utawala wa mpito.

Hata hivyo pande zote mbili zimekubaliana juu ya ajenda za kujadiliwa katika mzunguko wa pili, ambapo Brahimi alisema serikali ya Syria ilikataa maoni yake yaliyotaka kuanzwa kwa mazungumzo ya awamu ya tatu katika mjadala utakaolenga kupambana na ukatili, ugaidi, na baadaye kujadili serikali ya mpito.

Mzozo nchini Syria umegharimu maisha ya watu zaidi ya laki moja tangu ulipozuka mwaka 2011 mnamo mwezi March.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.