Pata taarifa kuu
UKRAINE

Wapinzani waitisha maandamano makubwa zaidi mwishoni mwa juma nchini Ukraine

Wapinzani nchini Ukraine wameitisha maandamano makubwa zaidi mwishoni mwa juma hili kuendelea kumshinikiza Rais wa nchi hiyo Viktor Yanukovych ajiuzulu. Kiongozi wa upinzani Arseniy Yatsenyuk amewaalika wananchi kushiriki maandamano ya jumapili katika viwanja vya uhuru mjini Kiev wakitimiza majuma matatu ya maandamano kupinga hatua ya serikali kushindwa kusani makubaliano muhimu ya ushirikiano na Umoja wa Ulaya EU.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Yanukovych kukataa kutia saini makubalino hayo umesababisha maandamano hayo ambayo ni makubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo toka mapinduzi ya chungwa ya mwaka 2004.

Rais Yanukovych ameendelea kuwa katika shinikizo baada ya polisi kushindwa kuwatawanya maelfu ya waandamanaji siku ya jumatano.

Katika mazungumzo na Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton, Rais Yanukovych aliahidi kusaini makubaliano hayo hivi karibuni licha ya kugoma kutaja tarehe ya kutekeleza suala hilo.

Umoja wa Ulaya umeahidi kuongeza msaada kwa nchi hiyo ikiwa mkataba wa ushirikiano na umoja huo utasainiwa.

Marekani imetishia kuiwekea vikwazo Ekraine baada ya maandamano hayo ambayo yalisababisha kujeruhiwa kwa makumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.