Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Hatimaye Wanadiplomasia waafikiana kuhusu mpango wa nyukli wa Iran kupitia majadiliano ya Geneva nchini Uswisi

Hatimaye Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani wamefikia makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran, Kiongozi Mkuu wa mjadala huo Bi, Catherine Ashton amethibitisha hilo baada ya takribani siku tano za majadiliano makali ya mjini Geneva nchini Uswisi. Mataifa yenye nguvu duniani ambayo ni Uingereza, Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Ujerumani wamekuwa na madai ya kutaka Tehran isitishe urutubishaji wa uranium ili iondolewe vikwazo inavyokabiliwa navyo.

REUTERS/Fabrice Coffrini
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema wamefikia muafaka wa mzungumzo hayo na miongoni mwa mambo muhimu kwao ni kutumia nyuklia katika uzalishaji wa nishati sambamba na kupunguzwa vikwazo vya kiuchumi.

Baada ya kutamatika kwa majadiliano hayo, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema kuwa makubaliano hayo yatahakikisha usalama wa Israel pamoja na eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa upande wake Rais wa Marekani Barack Obama amepongeza hatua hiyo ya kihistoria na kusema ni hatua kubwa ya kwanza kuelekea mpango wa kuimarisha usalama wa dunia kutokana na makubaliano hayo kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Hata hivyo Obama ameonya kuwa endapo Iran haitatekeleza vipengele vya makubaliano hayo, basi vikwazo vya takribani dola za Marekani bilioni 7 vitarejeshwa na shinikizo kuongezwa.

Iran ilikuwa ikishikilia msimamo wa kutokubali mapendekezo hayo kwa madai yanakiuka haki na maslahi ya Taifa lake ambalo linatumia teknolojia hiyo katika matumizi sahihi.

Wanadiplomasia wanaona kuwa kufikiwa kwa makubaliano hivi sasa ni hatua kubwa kutokana na mafahari hao kushindwa kukaa pamoja kwa takribani muongo mmoja.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.