Pata taarifa kuu
GENEVA-Mazungumzo

Mkuu wa wazungumzaji wa Iran asema kutoaminiana ni kikwazo cha maafikiano ya mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran

Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Geneva Abbas Araghchi ameonya alhamisi juu ya kutokuaminiana kama moja ya kikwazo cha mazungumzo hayo yahusuyo nyuklia kati ya mataifa makubwa duniani na nchi ya Iran.

Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Geneva Abbas Araghchi ameonya alhamisi juu ya kutokuaminiana kama moja ya kikwazo cha mazungumzo
Mjumbe mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Geneva Abbas Araghchi ameonya alhamisi juu ya kutokuaminiana kama moja ya kikwazo cha mazungumzo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kikwazo cha kutoaminiana kimekuwa kikwazo kikubwa hasa katika majadiliano ya mwisho na kuona kuwa ikiwa suala la kukosekana kwa kuaminiana haitawezekana kuendelea na mazungumzo yenye tija kama alivyonukuliwa Abbas Araghchi akisema katika televisheni ya taifa hilo.

Hayo yanakuja wakati huu ambapo Wanadiplomasia kutoka pande mbili wanaingia kwa undani zaidi alhamisi hii kujadili juu ya kupatikana kwa makubaliano kuhusu Nyuklia ya Iran.

Wanadiplomasia hao kutoka, Marekani, Uingereza, ufaransa, Urusi China, Ujerumani pamoja na Iran, wamekutana Geneva nchini Uswisi katika awamu ya tatu ya mazungumzo yaliyoanza tangu mwezi Octoba.

Kiongozi wa Ujumbe wa Iran katika mazungumzo hayo ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa serikali Mohamed Javaz Zarif pamoja na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton watachambua kwa undani zaidi na kuzingatia Nakala waliokubaliana Novemba 9.

Hivi karibuni rais wa Marekani Barack Obama aliwataka wajumbe wa baraza la Congress kutokazia kamba ya vikwazo zaidi kwa Iran baada ya serikali ya rais Rohani kuonyesha nia ya kupatikana muafaka.

Wachambuzi wa siasa wanaona ni jambo la Busara sana kufikiria upya vikwazo hivyo vya Iran.
Majaribio kadhaa yamegonga mwamba katika kutafuta suluhu ya mzozo huo kwa takribani muongo mmoja uliopita licha ya uchaguzi wa mwaka huu ambapo raisi Hassan Rouhan aliibuka mshindi wa kiti cha uraisi na kuonesha matumaini ya kufanikiwa kufikiwa tamati ya mzozo wa nyuklia ya Iran.

Hata hivyo nchi hiyo ikiwa bado inakabiliwa na vikwazo,tangu raisi mpya Rouhani kuingia madarakani mwezi August na kusimamisha shughuli za uzalishaji wa madini ya Uranium kwa mara ya kwanza.
 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.