Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry aalikwa kushiriki mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran mjini Geneva

Mpatanishi wa kimatiafa wa mazungumzo ya amani kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, Catherine Ashton, amemwalika Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kuhudhuria mazungumzo ya hii leo mjini geneva. Licha ya ratiba ngumu aliyokuwa nayo Kerry, amekubali mwaliko wa Mwanadiplomasia huyo wa Umoja wa Ulaya EU kushiriki mkutano huo ambao ni wa pili kufanyika toka Rais wa sasa wa Iran, Hassan Rouhani aingie madarakani mwezi Agosti mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imekuwa ikisisitiza kuwa ni lazima nchi ya Iran ishirikiane na jumuiya ya kimataifa katika kupata suluhu ya mzozo uliopo kabla ya kuondolewa vikwazo na kwamba uwajibikaji kwa nchi ya Iran ndio unaotakiwa kushuhdiwa kwasasa.

Mkutano huo unawakutanisha Maofisa wa serikali ya Iran na wawakilishi toka Marekani, Uingereza, China, Ufaransa, Urusi na Ujerumani.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakiishuku Iran kuwa inatafuta uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia kupitia mpango wake huo lakini Tehran imekuwa ikikanusha na kusema kuwa lengo lao ni matumizi salama pakee.

Wakati huo huo Wiziri ya mambo ya nje ya Ufaransa imethibitisha kuwa Waziri wake Laurent Fabius atahudhuria katika kikao cha ijumaa hii mjini Geneva.

Iran kwa upande wake ina matumaini huenda makubaliano yakafikiwa kupitia mkutano huo, ingawa imeweka wazi kuwa haitakubali kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium badala yake inaweza kutekeleza baadhi ya maswala yanayozungumziwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.